Na Sultani Kipingo


Mwanamuziki Luizer Nyoni  Mbutu ambaye Mei 11, 2022 ameandika historia mpya kwa kuwa mwanamke wa kwanza nchini kushinda nafasi ya Mwenyekiti Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA), leo annaandika ingine.


Historia  anayoiandika Luizer leo ni kuongoza na hatimaye kufanikisha maandalizi ya Sherehe za Miaka 37 ya CHAMUDATA, jambo ambalo halikuwahi kufanywa hata sikui moja na kiongozi yeyote wa chama hicho Hugo nyuma.


Sherehe za kuadhimisha mwaka 37 ya CHAMUDATA zinafanyika leo Jumatano January 11, 2022 kuanzia saa 12 jioni patika Ukumbi wa Gwambina Lounge, zamanı maarufu kama TCC Club Chang’ombe jijini Dar es salaam. HAKUNA KIINGILIO.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa CHAMUDATA, Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt Kedmon Mapana ndiye atayekuwa Mgeni Rasmi, kaaika sherehe hizo zilizoanzia mwishoni mwa juma kwa Michezo ya Netball na Soka iliyopambwa na wanamuziki na wadau wa Muziki.


Wanamuziki na wadau wengi wa Muziki wamemwagia sofa Luizer pamoja na viongozi wote wa CHAMUDATA kwa kusimama Kadete katika kurejesha mshikamano na uelewano baina ya wanamuziki na wadau wa Muziki, embat ulipotea hugo nyuma na kuleta sintofahamu kiasi iakwa haijulikani kiongozi ni nani na nini dira fake ya maendeleo ya tasnia.


Wadau hao wa Muziki wamefurahi kusikia kwamba kaika sherehe hizo leo Mgeni rasmi ni Dkt. Kedmon Mapana, msomi aliyebobea katika sanaa, akitokea chuo kikuu cha Dar es Salaam.


“Huyu (Dokta Mapana) Utamwona kama fala fulani hivi lakini kila baya na zuri katika sanaa  na hata muziki wa Tanzania analijua na hivi sasa yuko katika utafiti wa hali ya juu kuangalia njia za kisomi za kupambana na hatimaye kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizopo katika tasnia hii”, alisema mdau wa Muziki Juma Nassoro wa  Kariakoo jijini Dar es Salaam.Katika  uchaguzi mkuu  wa CHAMUDATA uliofanyika ukumbi wa Dar Modern ulioko Magomeni Mikumi mtaa wa Ifunda jijini Dar es Salaam, ulimshuhudia Luizer mwimbaji tegemeo na mwanamuzikio wa siku nyingi wa Twanga Pepeta, akiwashinda kwa mbali wapinzani wake Mwinjuma Muumini (aliyeshika nafasi ya pili) na Said Kaunga.

Mwimbaji wa Sikinde Original, Abdallah Hemba alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti aliyokuwa akiipigania na mwanamuziki mkongwe wa Tabora Jazz, Ramadhani Kitenge.

Katika nafasi ya Katibu Mkuu meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti alimbwaga  kwa Mali sana Hassan Msumari aliyekuwa akitetea kiti chake.

Katibu Msaidizi wa Chamudata aliibuka wakili msomi Baraka Elias Sulus ambaye alikuwa mgombea pekee na hivyo kura za ndio zikampitisha kwa kishindo, japo yeye mwenyewe hakuwepo ukumbini.

Nafasi sita za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji zilizokuwa na mchuano mkali, zikaenda kwa Profesa Abuu Omar, Cecy Jeremiah Logome Mwasi Kitoko, Bernedict Berno Sanga, Said Mdoe, Gabriel Bakilana na Rhobi Chacha. Wagombea wengine Matei Joseph, Shomary Ally, Tabu Mambosasa, Andrew Mwampashi na Sholinda Mwezimpya kura hazikutosha.

Uchaguzi wa Chamudata ulifanyika kwa uwazi wa hali ya juu chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Kamanda Mstaafu Jamal Rwambo (SACP) na kufanya zoezi hilo likamilike bila malalamiko ya upande wowote.

Hiyo ilijidhihirisha pale wagombea walioshindwa wote walipojitokeza meza kuu na kutia Saini fomu za matokeo  na walipopewa nafasi ya kusema machache baada ya uchaguzi walikubali matokeo na kupongeza mchakato mzima wa uchaguzi huo ulivyofanyika.

SAFU YA UONGOZI CHAMUDATA NI HII HAPA:

MWENYEKITI
Luizer Morris Nyoni

MAKAMU MWENYEKITI
Abdallah Hamis Hemba

KATIBU MKUU
Said Nassoro Kibiriti

KATIBU MSAIDIZI
Baraka Elias Sulus (Advocate)

WAJUMBE (NAFASI SITA):
1. Abbu Omar Abubakar
2. Cecy Jeremiah Lugome
3. Said Abdillahi Mdoe
4. Bernedict Berno Sanga
5. Gabriel Byabato Bakilana
6. Rhobi Abubakari Chacha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...