Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Ni rasmi Fainali ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2023 itawakutanisha Singida Big Stars kutoka Tanzania Bara dhidi ya Mlandege FC ya visiwani Zanzibar, Mlandege wamefuzu hatua hiyo baada ya ushindi wa jumla ya mikwaju ya Penalti 5-4 dhidi ya Namungo FC baada ya sare ya bao 1-1 kwenye dakika 90’.

Katika mchezo huo wa Nusu Fainali ya pili, iliyopigwa kwenye dimba la Amaan, Zanzibar, Namungo FC walianza kupata bao lao kupitia kwa Mshambuliaji Ibrahim Abdallah Mkoko kwenye dakika ya 7’ huku Mshambuliaji wa Mlandege FC, Bashima Saite akisawazisha katika dakika ya 45+5’.

Baada ya kuhitimishwa dakika 90’, timu hizo zililazimika kwenda kwenye changamoto ya mikwaju ya Penalti ambapo Mlandege FC walipata Penalti 5 dhidi ya Penalti 4 za Namungo FC.

Januari 13, 2023 kwenye dimba hilo la Amaan, Singida Big Stars watawavaa Mlandege FC majira ya Saa 2:15 Usiku ikiwa ni Fainali ya mashindano hayo ya Mapinduzi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...