Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
 KIUNGO Feisal Salum Abdallah (Feitoto) ameendelea kuzua mijadala kwa wadau wa mchezo wa soka nchini baada ya kuonekana akiwa katika ardhi ya Falme za Kiarabu akifanya mazoezi kwenye moja ya Kituo ambacho hakijafahamika jina lake kwa haraka.

Feitoto amechapisha baadhi ya picha akifanya mazoezi hayo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwa ni siku kadhaa tangu kudaiwa kuvunja mkataba na Yanga SC na kuondoka kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo Avic Town,Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Kupitia chapisho lake katika mtandao wa Twitter, Feisal amesema: “Haina kufeli, hakuna kukata tamaa tuzidi kuzikimbilia ndoto zetu, Mwaka Mpya.” Ujumbe huo unaweza kuwa ni ishara ya Mwanasoka huyo wa Kimataifa wa Tanzania, kwa sasa kuamua kubadilisha mazingira na kuchagua kucheza soka nje ya mipaka ya Tanzania.

Hata hivyo, Feisal huenda labda akasajiliwa na moja ya timu za Falme za Kiarabu kutokana na kiwango chake bora alichokionyesha muda wote akiwa Yanga SC. Feisal alidumu katika Kikosi hicho cha Wananchi akicheza nafasi ya Kiungo hususani Kiungo cha Ushambuliaji na mara nyingi amehusika kwenye upachikaji wa mabao katika Klabu hiyo.

Desemba 24, 2022 Feisal alichapisha ujumbe kwenye ukurasa zake za mitandao ya kijamii akiwaaga Wananchi baada ya kudaiwa kuvunja mkataba wake na timu hiyo, licha ya Wananchi wenyewe kudai kuwa Kiungo huyo ana mkataba Klabuni hapo hadi ifikapo mwaka 2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...