NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza

BARAZA Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza kwa hisani ya kampuni ya Rock Solution limeandaa chakula cha mchana cha watoto yatima kusheherehea mwaka mpya.

Yatima hao zaidi ya 200 kutoka vituo tofauti jijini Mwanza,wamehudhuria hafla ya chakula hicho leo kukiwa na kauli mbiu ya tuwapende yatima tuwasaidie yatima kwani hatujui kesho mwanao atasaidiwa na nani?

Akizungumza kabla ya chakula hicho leo Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke ameitaka jamii kuwalinda,kuwalea na kuwathamini watoto yatima kutokana na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa na watu wasio na hofu ya Mungu.

Amesema waumini wa dini ya kiislamu na wasio na waislamu wengi wametawaliwa na ubinafsi wa kuishi na watoto wao pekee,hivyo aliwaasa wawasaidie yatima kwani hawafahamu lini watoto wao watakuwa yatima na watasaidiwa na nani kesho.

“Anayemsaidia yatima atakuwa bega kwa bega na Mtume Muhammad peponi,leo sisi biashara imeharibika sababu tumegeukia kuchanjwa chale tumewasahau yatima na nyumba inayomfanyia vizuri yatima hung’aa mbinguni,”amesema Shekhe Kabeke.

Pia,kiongozi huyo wa kiroho amekemea vitendo vya ukatili na ulawiti wanavyofanyiwa watoto wakiwemo yatima na kuwanyooshea kidole wazazi kuwa wamesahau wajibu wa malezi ya watoto huku akiwataka waislamu na wasio waumini wa dini hiyo kuchukua mtoto mmoja yatima na kumlea ili kupata thawabu kwa Mweyezi Mungu.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Rock Solution,Zakaria Nzuki ameeleza kwa zaidi ya miaka mitano sasa amekuwa akitoa sadaka ya kuandaa chakula kwa ajili ya watoto yatima ikiwa ni sehemu ya mchango wa kampuni wa kurejesha faida kwa jamii ya wasiojiweza wakiwemo yatima.

Amesema kuwa ameguswa kuwasaidia yatima hao wajione sawa na watoto wengine na kukosa wazazi hakuwaondolei haki ya kuishi kwa upendo na heshima kwenye jamii na mazingira magumu wanayoishi yasisababishe wasifanikiwe,uwe mwanzo wao kuzungumzia historia yao.

“Nimepitia mazingira hayo baada ya kufiwa mama yangu na nimejifunza mengi kwa watoto hawa,magumu wanayopitia si kwa bahati mbaya na kama Mungu hajayaruhusu hayawezi kutokea na kampuni yangu imejengwa na wao,”amesema Nzuki.

Mkurugenzi huyo wa Rock Solution alisema baadhi ya vituo yatima wa shida nyingi na huko ndani hakuna mtu wa kuwatembelea,kuwasilikiza na kufahamu mazingira wanayoishi na changamoto zao,hivyo jamii ikapata fursa ikawaone na kuwaombea walezi wao.

“Kituo utakuta kina watoto 108 na wanakopita ni sehemu ya moto sawa na chuma,wana changamoto nyingi ikiwemo ya kuugua,nimekuwa wakala wa watoto yatima baada ya kufahamu mazingira wanayoishi suluhu ni kuwataia bima za afya na Mungu amenijali ingawa kila kinachopitia kwangu si mali yangu hata fedha ninazopata si zangu ni za watumishi,”amesema Nzuki.

Ameisihi jamii kama wazazi kujifunza kinachofanywa na Rock Solution kusaidia yatima na kuahidi kumsomesha Al-Badh Yusuph, pia kampuni hiyo inagharamia masomo ya wengine zaidi ya 60 kwa mapato yake huku wawili waliohitimu chuo kikuu wameajiriwa kwenye kampuni.

Awali mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shle ya sekondari Angeline Mabula, Al-Badh Yusuph amewaonya waumini wa dini ya Kiislamu,jamii na wananchi kutowapatia haki yatima,kuwatendea kinyume na utu,kuwadhulumu na kula mali zao ni miongoni mwa dhambi saba zinazoangamiza nafsi.

Amesema dhambi zinazoangamiza nafsi ni kudhulumu na kula mali za yatima,kuwanyima haki za msingi na kuwatendea kinyume na utu kunawasononesha na kusababisha wawakumbe wazazi wao,hivyo jamii iwapende na kuwahudumia watoto yatima.

“Mtume Muhammad S.A.W anasema katika Kuran,katika Uislamu hakuna nyumba nzuri kama inayoishi na yatima na kumpa stahiki zake,watu wanaodhulumu na kula mali zao na kutopatia haki yakiwemo mahitaji ya msingi,wanajipalia moto mkali wala wasijione wamefaulu kwa kuwadanganya wakikua watazikuta,”amesema Yusuph.

Amewasistiza kutowapatia yatima haki zao kunawafanya wawakumbuke wazazi wao wala hakuna malipo mazuri zaidi ya kuishi na yatima na yeyote anayemridhisha kwa kugusa kichwa na kushika nywele zake Mwenyezi Mungu humlipa kila nywele aliyoshika.

Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke,akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu kwenye hafla ya chakula cha mchana cha watoto yatima kilichoandaliwa na BAKWATA mkoani humu kwa hisani ya kampuni ya Rock Solution ili kusherehekea mwaka mpya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...