Na John Walter-Manyara

Waamini na watu wote wenye mapenzi mema wametakiwa kuiombea miito mitakatifu ndani ya familia ili injili ya kristo, iwafikie wale wote ambao hawamtambui kristo.

Hayo yamo katika homilia takatifu, iliyotolewa na askofu wa jimbo Katoliki la mbulu Mhashamu Askofu Anton Lagweni wakati wa adhimisho la sadaka ya misa takatifu ya kutoa daraja ya ushemasi iliyofanyika katika kanisa la Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Parokia ya Sanu Jimbo Katoliki la Mbulu Januari 5, 2023.

Askofu Lagweni amesema kuwa shemasi anapokea paji la roho mtakatifu kwa ajili ya kupeleka neno la mungu kwa watu,na hivyo anapaswa kujitoa sadaka kwa ajili ya watu wa Mungu.

Akitoa salamu za pongezi, Mbunge wa jimbo la Mbulu Mjini Zakaria Paul Issay amewapongeza mashemasi hao kwa kuitikia sauti ya Mungu huku akitoa wito wa kuendelea kuwaombea ili waweze kutimiza wito huo wa ukuhani walioitiwa.

Mashemasi waliopokea daraja hiyo ni shemasi Paulo John Pissa kutoka Parokia Ndogo Ya Bargishi Uwa Mbulu, Frateri Anton Baloho kutoka Parokia ya Geklum Lambo Karatu, Frate Paskali Bombo kutoka parokia ya Kateshi Hanang, Shemasi Joakimu John Baran wa parokia ya Karatu,Shemasi John Masawe wa Parokia Ya Gitting, Shemasi Faustine Joseph wa Parokia ya Kiru.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...