KAMPUNI ya Dough Works Limited katika imeendelea kutoa fursa kwa watanzania katika masoko ya ndani, kama wazalishaji wa kuku, kuongeza nafasi za ajira kwa kuongeza ajira nchini Tanzania.

Kampuni hiyo imetoa ajira za moja kwa moja kwa takriban Watanzania 750 ambao kupitia kazi zao wanakidhi mahitaji yao na kuendeleza maisha yao ya kila siku.

Mkurugenzi Mkuu wa Dough Works, Vikram Desai ameyasema hayo leo Januari 23, 2023 wakati wa kufungua Mgahawa wa nane wa KFC na Mgahawa wa tisa wa Pizza Hut katika Jengo la Himo lililopo Mbezi Beach jijini Dar Es Salaam. Amesema kuwa watu wengi wameajiriwa kama wapishi, watumishi, wahasibu, wasimamizi wa majukumu na wasambazaji wa chakula kwa watu, huku ikidumisha na kutoa chakula cha ubora wa juu na uzoefu unaofaa zaidi kwa watumiaji kila Uchwao.

Akizungumza katika Ufunguzi huo amesema kwa kurudisha mafanikio kwa jamii na kufungua milango kwa watoto 54 wenye mahitaji maalum wanaotunzwa na Baba Oreste Foundation walioalikwa kufurahia Chakula cha mchana cha pizza na kuku kutoka kwenye mgahawa huo wa Mbezi Beach.

“Ni furaha kuwakaribisha wageni wetu mbalimbali ambao ni waheshimiwa, washirika, wadau na wafanyakazi wetu katika mgahawa wa Pizza Hut & KFC iliyopo pamoja ambayo ina sehemu kubwa ya kukaa, sehemu ya kucheza ya watoto, kwa ajili ya wateja wetu, pia mgahawa huu utakuwa na gari ambalo litahudumia wateja wetu wote wa karibu na maeneo yafuatayo Mbezi Beach, Kunduchi, Goba, Mbezi Juu, Africana, Bahari Beach na Kilonga Wima.” Ameeleza

Kampuni hiyo ya Sekta ya utoaji huduma ya chakula inatarajia kuendelea kuandaa hafla hizo na kushirikiana na mashirika yanayochangia kuinua jamii na ustawi wa Jumuiya ya Mbezi Beach.

Kwa kufunguliwa kwa migahawa mipya ya KFC na Pizza-Hut inajivunia ushirikiano wa kukuza migahawa ya Kitanzania kufikia viwango vya kimataifa vya kutoa huduma bora na huduma za kiwango cha kimataifa.

Kwa Upande wa Naibu waziri wa zamani katika serikali ya awamu ya tatu, Lita Mlaki amewashukuru Kampuni ya Dough Works kwa Kufanya Uwekezaji katika Jengo la Himo Plaza hiyo itakuwa fursa kwa wakazi wa Mbezi Beach kupata huduma ya chakula kwa karibu zaidi.

Amesema amesema kuwa Jengo hilo bado lina nafasi za wawekezaji wengine kwenda kuwekeza kwa jengo hilo lipo katika eneo zuri la kibiashara.

Kwa Upande wa Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Dough Works, Shafii Idegge amesema kuwa Uwekezaji zaidi utaenda kufanyika katika Mikoa ya Dodoma, Arusha na Zanzibar hivyo wananchi wakae Mkao wa Kula kwani mazungumzo yanaendelea ili kuwekeza katika mikoa mingine tofauti na Dar es Salaam.

Akizungumzia kuhusiana na ufanisi wa Kampuni ya Dough Works amesema kuwa Watanzania zaidi ya Mia Saba tayari wamepata ajira katika Migahawa ya KFC nane na Piza Hut tisa iliyopo jijini Darbes Salaam na ajira zaidi zitaenda kuongezeka kwa mikoa mingine ambapo Mgahawa huo utaenda kufunguliwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Dough Works, Vikram Desai akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23, 2023 wakati wa kufungua Mgahawa wa nane wa KFC na Mgahawa wa tisa wa Pizza Hut  katika Jengo la Himo lililopo Mbezi Beach jijini Dar Es Salaam(Watatu kutoka Kulia.)
Mkurugenzi Mkuu wa Dough Works, Vikram Desai akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23, 2023 wakati wa kufungua Mgahawa wa nane wa KFC na Mgahawa wa tisa wa Pizza Hut  katika Jengo la Himo lililopo Mbezi Beach jijini Dar Es Salaam.


Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgahawa wa KFC na Pizza Hut wakishiriki chakula cha Pamoja na watoto wenye mahitaji maaalumu wa kituo kilichopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Dough Works, Vikram Desai akifurahi pamoja na wageni waalikwa katika ufunguzi wa Mgahawa wa nane wa KFC na Mgahawa wa tisa wa Pizza Hut  katika Jengo la Himo lililopo Mbezi Beach jijini Dar Es Salaam leo Januari 23, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...