Na Khadija Seif,Michuzi TV 

MABONDIA 18 wanatarajia kusindikiza pambano kubwa la ngumi litakalomhusisha bondia maarufu nchini Seleman Kidunda dhidi ya bondia raia wa Democrasia ya Congo Patrick Mukala.

Aidha kutokana na uwepo wa mabondia hao vijana, mashabiki wa mchezo wa ngumi wwmeombwa kutazama vipaji vya mabondia wachanga  mtaani ili wapewe nafasi ya kuonekana  ili kubadilisha mchezo wa Masumbwi na kuwa na Mabondia wengi wenye mafanikio na majina nje na ndani ya nchi.

Akizungumza Dar es Salaam  Promota wa Mapambano ya ngumi za kulipwa nchini kutoka KampuniyaKemmon sports Agency, Saada Kasonso amesema wadau na wapenzi wa ndondi wategemee kuona vipaji vipya vya mabondia kutoka Mtaani hususani mabondia wachanga.

“Katika pambano linalokuja ambapo pambano kubwa ni Selemani Kidunda dhidi ya Patrick  Mukala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uzito wa kilo 76 wakigombania mkanda ABU  raundi 10  litasindikizwa na vijana wapya ambao wana uwezo mkubwa japo  walikosa nafasi ya kuonekana kupitia kampuni yetu ya Kemmon Sports Agency, tutawatambulisha vipaji hivyo kwa watanzania".

Saada amewataja mabondia 18  ni Oscar Richard dhidi ya Adam Mbega,  Emmanuel Mwakyembe atapigana na Francis Miyeyusho, Mbaraka Mtange atazichapa na Hamza Mchanjo, Alex Kachelewa dhidi ya Adam Mrisho, Mwinyi Mzengela kumenyana na Ajemi Amani.

Wengine Abdul Kubila dhidi ya Msabaha Salum, Omary Baraka kupigana na Muksini Kizota, Ahmady Pelembela dhidi ya Iddy Pazzy wakati Frola Machela atacheza na Halima Bandola.

Akizungumzia pambano hilo, Bondia Selemani Kidunda amesema kutokana na maandalizi mazuri anayofanya, watanzania wategemee ushindi kutoka kwake.

“Nimejipanga na naendelea na mazoezi, bondia ninayeenda kucheza naye ni mzuri, lakini atapigwa na mkanda utabaki nyumbani."

 Kidunda mwenye umri wa miaka 39, anapanda ulingoni akiwa na kumbukumbu ya kushinda pambano ya Kidemkrasi ya Congo (DRC), pambano hilo lilofanyika Julai mwaka jana, Songea mkoani Ruvuma.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...