*Asema huu si wakati wa kulipa kisasi, ahimiza umoja, mshikamano


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV-Mwanza

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)kimeanza rasmi kufanya mikutano yake ya hadhara huku ikitumia nafasi hiyo kuelezea kwamba huu ni wakati wa kujengwa Taifa lisilo la kisasi wala kuumiza viongozi wa vyama, wanachama au wafuasi wa chama chochote.

Aidha Chadema imeelezea hatua mbalimbali ya madhila na mateso ambayo wanachama wa Chadema na wa vyama vingine wameyapitia katika kipindi cha miaka saba ya uongozi wa Serikali lakini wanamshukuru Mungu kwa kufika siku ya leo.

Akizungumza kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema anaposimama mbele ya wananchi hao ni baada miaka saba ya kifungo haramu kilichokiuka Katiba na Sheria za nchini.

“ Vombo vyote vya ulinzi na usalama vya taifa vikaheshimu ubatili wa Katiba na Sheria, sauti za viongozi, sauti za wananchi zilizimwa kwa miaka saba.Kwa hiyo ndugu zangu wana Chadema, ndugu zangu msiokuwa wana Chadema napozungumza nanyi hapa namshukuru Mungu wetu ambaye amekuwa wa baraka.

“Awe Mungu wa Waislamu, Mungu wa Wakristo awe Mungu wasio na dini, Mungu amekuwa baraka katika nchi yetu kwani ameweza kutuvusha hatua kwa hatua hadi tufakika siku ya leo tunapoyazungumza bila kujali imani ya yoyote miongoni mwetu.

“Leo tunapozungumza mustakabali wa nchi yetu bila kuhofu kauli ya yoyote aliyetangulia kabla yetu lazima tushukuru Mungu wetu kwasababu taifa hili limepitia mapito mengi na leo nitazungumza mapito machache sio yote. Nitazungumzia mapito ya miaka saba iliyopita chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano yaliyogeuza taifa hili ,yaliyogeuza mafanikio yote tuliyopata kama taifa na kuligeuza taifa hili kuwa taifa la mateso, maumivu, misiba.”

Mbowe ametumia nafasi hiyo kueleza yote yaliyotokea anachukua nafasi hiyo bila kujali itikadi za vyama na binafsi anatamua miongoni mwao wako wanachama Chadema, CCM, wanachama wa vyama vingine na wasio na vyama wote waliumizwa na maumivu yaliyosababishwa na viongozi wa taifa hili.

“Wanachama wa Chadema waliumizwa na wako walioumizwa zaidi , wako wana ccm walioumizwa na wako wana ccm waliokuwa faidika wa uovu uliofanyika. Wako wana chama wa vyama vingine na wasio nao na vyama nao waliumizwa.

“Taifa letu halipaswi kuwa taifa la kuumiza kiongozi yoyote, mwanachama yoyote , mfuasi yoyote wa chama chochote.Taifa letu linapaswa kuwa la watu walioungana, wanaoshikamana , wanaosimama katika misingi ya demokrasia, misingi ya utawala wa sheria na misingi ya haki kwa wote.

Amesisitiza kuwa pamoja na yote ambayo yametokea Chadema haitalipa kisasi kwa yoyote huku akiendelea kueleza umuhimu wa kuwa kujenga taifa lisilo na kisasi bali liwe na mshimakano wa kitaifa.“Kwa hiyo ndugu zangu nimetaka nizungumze mambo hayo ya msingi sio msingi wa Chadema , sio msingi wa Mbowe lakini msingi wa taifa.”


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...