Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dodoma Alhaj Adam
Kimbisa amesema hatua aliyochukua Rais Samia Suluhu Hassan ya kutengua
katazo la mikutano ya hadhara inathibitisha ukomavu alionao , weledi,
uthubutu na nia nzuri ambayo kwa Watanzania.

Alhaj Kimbisa ameyasema hayo leo Januari 5,2023 jijini Dar es Salaam
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua iliyochukuwa
na Rais Dk.Samia kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa
nchini.

“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alikutana na viongozi wa vyama vyote vya
siasa ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa jitihada ambazo amekuwa
akizifanya tangu aingie madarakani za kuhakikisha mazingira ya
ufanyaji siasa yanaboreshwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha hali ya
demokrasia , uhuru wa vyombo vya habari , uhusiano na vyama vya siasa
pamoja na uhuru wa kujieleza.

“Ni ukweli kuwa jitihada , nia na uthubutu wake sit u umekuwa nguzo
muhimu ya kuchochea kasi ya mariadhiano ya kisiasa nchini bali
zimechangia pakubwa kuondoa mkwamo wa kisiasa ulioshuhudiwa kwa miaka
sita sasa.Hatua iliyochukuliwa na Rais Samia kuruhusu mikutano ya
hadhara kwa vyama vya siasa inathibitisha ukomavu alionao,”amesema
Kimbisa.

Amesema CCM Mkoa wa Dodoma kinaamini kuruhusiwa kwa mikutano ya
hadhara kutaimarisha nguvu za kisiasa za Chama hicho, kutapanua wigo
kwa wanachama wengi zaidi kutoa mawazo chanya kuhusu masuala
yanayohusu Taifa lao na kufungua fursa kwa viongozi wa ngazi wa Chama
wa ngazi zote kunadi na kutangaza hadharani mazuri yote
yanayotekelezwa na Serikali.

Aidha amewaomba watanzania wote kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.Samia
, kumuombea afya kwa Mungu , busara na maono zaidi ili aendelee
kulifanyia Taifa mambo makubwa zaidi.

“Ni dhahiri kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake amefanya
mambo makubwa kwenye sekta ya miundombinu , afya , elimu , ulinzi na
usalama, demokrasia , uhusiano wa kimataifa pamoja na uhuru wa vyombo
vya habari,”amesema Alhaj Kimbisa.

Ametumia nafasi hiyo kueleza wana CCM Mkoa wa Dodoma wanamuahidi Rais
Samia na Watanzania kwa ujumla kuwa watafanyasiasa za kistaarabu
zisizo na lugha za maudhi , vurugu , maandamano yasiyo na lazima ili
kuonesha ukomavu wa kisiasa kwa maslahi mapana ya nchi.

Mwenyeiki wa CCM mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Januari 05,2023 wakati akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuondoa zuio la mikutano ya kisiasa ya hadhara nchini. 

PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG


Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mwenyeiki wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaj Adam Kimbisa alipokuwa akizungumza nao leo Januari 5,2023 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya kisiasa nchini.
Mbunge wa jimbo la Chemba Mh Mohammed Lujuo Moni akizungumza jambo mbele ya Waandishi wa habari leo jijini Dar akiunga mkono tamko la Mwenyekiti wa CCM Dodoma,la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya kisiasa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...