Prudencia Paul Kimiti
ametembelea na kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika vituo vya
kulelea Watoto yatima vya Peter's House Bangwe na Katandala Orphanage
Center.
Kituo cha kwanza alichotembelea ni kituo cha Peter's
House kilichopo Kata ya Izia mtaa wa Bangwe ambapo katika kituo hicho
Prudencia alitoa vifaa vya shule kwa wanafunzi ambao wanasoma shule
mbali mbali za serikali na binafsi wanaosomeshwa na kituo hicho.
Amekabidhi
madaftari ya kuandikia na Ma counter books kumtosha kila mwanafunzi,
kalamu za wino, kalamu za risasi na mikebe na alitoa Juice, Mchele na
kuacha pesa za kununulia nyama ili watoto waweze kula na kufurahi kwa
pamoja kama watoto wengine wanaoishi kwa wazazi wao.
Kituo cha
pili alichotembelea ni kituo cha watoto yatima cha katandala yaani
Katandala Orphanage Centre kinachopatikana Kata ya Katandala ambapo
Katika kituo hicho Prudencia alitoa msaada wa maziwa kwa watoto
wachanga, mkaa wa kupikia na kuacha pesa ya kulipia bili ya umeme.
Aidha,
alifarijika sana kuona wanafunzi wote wanaosoma katika vituo vyote
viwili kuwa na uwezo mkubwa wa kitaaluma katika masomo yao, na
alipowahoji baadhi yao walimueleza kuwa wanasoma kwa bidii ili waweze
kuwa madaktari na wengine Wanajeshi ili kuisaidia nchi na watu wake hapo
baadae.
Hata hivyo, Prudencia anatoa rai kwa wadau wa ustawi na
maendeleo jamii Mkoa wa Rukwa kuendelea kushirikiana na vituo hivi
ambavyo vinalea watoto waliobeba ndoto za kuisaidia nchi siku za usoni.
Pia, anawapongeza TRA Sumbawanga kwa kuwa karibu kusaidia mahitaji muhimu ya mara kwa mara katika kituo cha Peter's House.
Home
JAMII
PRUDENCIA PAUL KIMITI ATEMBELEA NA KUTOA MSAADA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU RUKWA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...