Na Said Mwishehe, Michuzi TV

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dk Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Wananchi wa India Shri Om Birla huku jambo kubwa likiwa kuendeleza ushirikiano kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya afya.

Akizungumza mbele ya Spika huyo wa Bunge la Wananchi wa India leo Januari 18,2023 katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam ,Dk .Tulia amesema kwamba ugeni wa Spika huyo ni wa kihistoria kwani imepita miaka 50 tangu ujio wa aina hiyo mwaka 1961.

Dk Tulia amesema wamezungumza mambo mengi ikiwemo ushirikiano wa kibunge kati ya Bunge la Tanzania na Baraza la Wawakilishi upande wa Zanzibari pamoja na Bunge la Wananchi wa India.

"Kwa hiyo tumepunguza kuhusu ushirikiano katika mambo mengi na kwa upande wa Bunge tumezungumza kuamsha uhusiano ulikuwepo kati ya Mihimili hii lakini kuweza kutumia chuo cha mafunzo ambacho wao wanacho.Mafunzo ambayo yanatolewa na Chuo hicho ni kwa ajili Wabunge pamoja na wafanyakazi wa Bunge la Wananchi wa India.

"Mambo mengine ambayo tumeyazungumza ni utayari wa Bunge la India kushirikiana na Baraza la Wawakilishi Kwa maana ya Zanzibar pamoja na kushirikiana na Bunge la Tanzania kwenye eneo hilo .Kuhusu nchi zao mbili katika ushirikiano uliopo tangu miaka ya 1960 ambapo India na kama mnavyofahamu inajulikana kama mama wa demokrasia.

"Lakini mwaka 1961 India ilileta hapa Ubalozi wake,ambapo Tanzania ilikuwa bado haijapata uhuru wake kwa maana ya kwamba ilipata Uhuru Desemba 12 mwaka wa 61.Wao walikuwa wameshakuja hapa nchini kwasababu ya wao kama watu wanaopenda demokrasia na walikuwa wameshapata Uhuru kabla walikuja hapa kwetu ili kushirikiana nasi katika mambo mbalimbali na tangu wakati huo nchi hizi zimeendelea kuwa na ushirikiano wa karibu katika sekta mbalimbali.

Akielezea zaidi Dk.Tulia amesema kuwa Serikali ya India imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo akitoa mfano Kwa upande wa Tanzania Bara kunatekelezwa mradi wa maji katika miji 28 ambao una thamani zaidi ya dola za marekani milioni 500 na India imetoa fedha hizo kwa ajili ya mradi huo uweze kukamilika.

"Kwa hiyo miradi ile inayotekelezwa kwenye miji 28 Serikali ya India imeshiriki kikamilifu kwa hiyo tunawashukuru sana.Mnafahamu mnafahamu mradi mkubwa wa maji wa kutoa maji Ziwa Victoria na kupeleka kwenye mikoa yetu ya Tabora, Shinyanga na mikoa ya karibu pia fedha zilitoka India walitoa dola za Marekani milioni 268 kama sehemu ya utekelezaji wa mradi ambao umekamilika na miradi hiyo imezinduliwa na Serikali yetu.

"Lakini eneo la afya ninyi ni mashahidi, Watanzania wengi wanaenda kutibiwa India pamoja na kwamba kuna mashirikiano ya hapa na pale kwa maana wakati mwingine madaktari wa India wanakuja hapa kushirikiana na madaktari wetu wa Hospitali kubwa kama Muhimbili kufanya upasuaji na baadae wanaondoka.

"Hivyo tumezungumza mashirikiano zaidi kwenye eneo hilo la afya kwasababu tunafahamu sio Watanzania pekee wanakwenda kwenye matibabu India , wanaenda na wengine wa nchi jirani, tunataka kuwa na mahusiano ya karibu ya afya ili teknolojia ya matibabu pia na madaktari waweze kutengeneza nazingira Tanzania iwe kitovu hata kwa jirani,kwa hiyo mambo mengi tumezungumza kati ya mambo ya kushirikiana.

Kwa upande wake wa Spika wa Bunge la Wananchi wa India Shri Om Birla ametumia nafasi hiyo kueleza masuala mbalimbali ambayo wameyazungumza na miongoni mwa sekta ambazo wamezungumza ni sekta ya kilimo,maji ,afya,na teknolojia huku akisisitiza kuhusu matumizi ya Teknolojia katika kilimo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Tulia Ackson ( wa pili kulia) akisalimiana na Spika wa Bunge la Wananchi la India Shri Om Birla (kushoto) baada ya kukutana katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo Januari 18,2023.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Tulia Ackson ( kushoto) akigonga glasi na Spika wa Bunge la Wananchi wa India Shri Om Birla (kulia) leo Januari 18,2023 baada ya kukutana kwa ajili ya kufanya mazungumzo yenye lengo la kujadili masuala mbalimbali

Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson akifafanua jambo baada ya kukutana na Spika wa Bunge la Wananchi wa India Shri Om Birla leo Januari 18,2023 jijini Dar es Salaam






Matukio mbalimbali kwenye picha baada ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Tulia Acksoni alipokutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Wananchi wa India Shri Om Birla leo Januari 18,2023 jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...