SERIKALI kupitia Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imewataka Watanzania kutoa taarifa pale ambapo wanahisi kuna udanganyifu unafanyika hasa katika maeneo yenye fukwe za bahari,bandarini kwenye fukwe za Ziwa pamoja na mipakani.


Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa fedha wa Mamlaka hiyo, Dinah Edward akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka TRA, Alphayo Kidata wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wakala wa Forodha ambayo hufanyika Januari 26 kila Mwaka ambayo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa kwa kutoa taarifa kutaifanya TRA kuweza kukusanya Ushuru na Kodi za Serkali.

Amesema kuwa TRA imekuwa ikijikita katika kuhamasisha wafanyabiashara kulipa kodi hivyo kukwepa kodi ni kinyume cha sheria na kanuni za serikali.

Pia amesema siku hiyo imewekwa kwaajili ya kuwaweka pamoja wanachama wa Wakala Wa Forodha ili kuangalia kwa pamoja fursa zilizopo duniani pamoja na kuona namna ambavyo mataifa mbalimbali yanafanya shughuli kwa uwiano sawa.

Kwa upande wake Kamishna wa forodha –TRA, Said Athman amesema katika kutekeleza mkataba wa kimataifa wa Wakala wa forodha tayari serikali imeanza kunufaika na biashara za kimataifa pamoja na kukuza pato la Taifa kupitia kodi.

Akizungumzia kuhusiana huduma mbalimbali zinazotolewa na TRA, amesemema kuwa Mamlaka hiyo ni nambari moja kwenye ubunifu, Automation na ufuatiliaji.

“Tumeiprove njia za ukusanyaji Mapato katika vituo mbalimbali vinavyotolewa huduma na TRA ikiwa na huduma za kijamii, Sisi wakala wa Forodha umetupatia Access za kuingia kwenye mifumo na kufanya Return Assessment.” Ameeleza

Naye Rais wa Chama cha mawakala wa forodha Nchini, Edward Urio ameiomba TRA kuwashirikisha walipa kodi katika utekelezaji wa mujukumu yao ili kuondoa kodi kinzani kwa wazalisha wa bidha mbalimbali.

Shirikisho la Wakala wa forodha Duniani lilianzishwa mwaka 1952 Nchini Ubelgiji, Tanzania ilijiunga mwaka 1964 lengo ni kujiweka katika nafasi za kimataifa ili kunufaika na misaada pamoja na mafunzo, misaada, ushirikishwaji, pamoja na vikao vinavyofanyika kimataifa.

Wanafunzi wa shule wakipokea Vyeti wakiwakilisha wanafunzi wenzao waliojiunga na Vilabu vya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ikiwa ni katika kueneza Uzalendo wa Kulipa Kodi kwa hiyari kwa wanafunzi hao.







Baadhi ya Wadau wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Wakala wa Forodha wakipokea Vyeti vyao vya kutambua Mchango wao katika Tasnia hiyo katika Maadhimisho ya Simu ya Kimataifa ya Wakala wa Forodha Duniani ambavyo hufanyika Kila Mwaka Ifikapo Januari 26.




Wadau wa Wakala wa Forodha wakiwa katika Picha ya pamoja katika Siku ya Kimataifa ya Wakala wa Forodha iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...