Baada ya ‘Follow Me’ aliyoshirikiana na Harmonize na ‘Mouzzah’ kutoka miezi miwili
iliyopita, nguli wa muziki nchini Tanzania Aslay anatarajia kuachia kazi yake
mpya iitwayo ‘Inauma’, ifikapo tarehe 27 Januari, 2023.
‘Inauma’
ni wimbo wa mapenzi lakini wenye kusikitisha na kuumiza moyo, wimbo huu una
mahadhi ya mpangilio wa ara za muziki wa zamani wa kitanzania utakaoweza kukupa
hisia kali sana. Katika wimbo huu, Aslay amezungumzia wivu, ambapo unapelekea
kushindwa kuvumilia pale unapoachwa na Yule umpendaye kwa dhati
Kama
ujuavyo Aslay ni mwandishi bora kabisa anafanya kazi kubwa ya kupangilia maneno katika tungo zake,katika uandishi huu
unaongeza utofauti kwenye wimbo, na kuweka ucheshi uliotumika unafanya wimbo
kuwa wakipekee vinginevyo ungekuwa wimbo wa mapenzi wa kusikitisha, lakini
ucheshi umenogesha na kuufanya wimbo wa kufurahisha na kuumiza katika mapenzi.
Aslay kwa sasa yupo chini ya lebo
kubwa ya muziki Afrika ijulikanayo kama Sony Music Africa na kazi zake
zikisimamiwa na Rock Star Africa. Hakika mwaka 2023 ni mwaka mwingine wa kijana
huyo kukonga mioyo ya mashabiki zake na wapenzi wa muziki wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...