Asasi isiyo ya Kiserikali ya Life and Hope Rehabilitation Organisation(LHRO) imetembelewa na viongozi wa CDC toka Makao Makuu yaliyopo Marekani huku wakifatana na viongozi wa CDC Tanzania na viongozi wa CDC toka Zambia na Msumbiji ambao walikuja Tanzania kuangalia kukagua miradi ya MAT unaoendelea katika kliniki za MAT  iliyopo katika hospitali za Muhimbili, Mwananyamala na Hospitali ya rufaa ya Temeke na walitembelea kliniki hizo na kujionea utendaji kazi wake.

Katika ziara hiyo maafisa toka Msumbiji na Zambia walipita walitembelea ofisi za Asasi za kiraia kujifundisha na kujionea wenyewe huduma za kuwaibua,waraibu wa dawa za kulevya,na jinsi wanavoadaliwa mpaka kupelekwa kliniki za MAT hasa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Life and Hope Rehabilitation Organisation(LHRO) iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika msafara huo waliambatana na wadau wanaojishughulisha na sekta ya afya wakiwemo toka Wizara ya Afya,MDH,THPS,AMREF,ICAP,NACP,DCEA(Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya.
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya Kiserikali ya Life and Hope Rehabilitation Organisation(LHRO) Al-karim Bhanji akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na asasi hiyo walipotembelewa na viongozi wa CDC toka Makao Makuu yaliyopo Marekani huku wakifatana na viongozi wa CDC Tanzania na viongozi wa CDC toka Zambia na Msumbiji ambao walikuja Tanzania kuangalia kukagua miradi ya MAT.
Baadhi ya wadau wakichangia mada mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya Kiserikali ya Life and Hope Rehabilitation Organisation(LHRO) Al-karim Bhanji walipotembelea miradi pamoja na ofisi za Asasi hiyo iliyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya Kiserikali ya Life and Hope Rehabilitation Organisation(LHRO) Al-karim Bhanji akitoa zawadi kwa baadhi ya viongozi wa CDC toka Makao Makuu yaliyopo Marekani, viongozi wa CDC Tanzania, viongozi wa CDC toka Zambia na Msumbiji ambao walikuja Tanzania kuangalia kukagua miradi ya MAT mara baada ya kutembelea ofisi za asasi hiyo jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...