Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam Nikita Arragawal akimpa mkono Mkuu wa wilaya Saad Mtambule  pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Minanzini kama ishara ya kukamilika kwa zoezi la ugawaji wa Madawati pamoja na zoezi la upandaji miti.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule akizungumza machache mara baada ya kupokea Msaada wa Madawati 200 yenye thamani shilingi milioni 30 kwa Klabu ya Rotary dar na kuwakabidhi shule ya msingi Minanzini Kata ya Mwananyamala B Jijini Dar es salaam
Mkuu wa wilaya Saad Mtambule akiwa pamoja na Rais wa Klabu ya Rotary Dar wakiendelea na zoezi la upandaji wa miti katika shule ya msingi Minazani iliyopo Kata ya Mwananyamala B Jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea msaada wa Madawati 200 yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 ikiwa ni sehemu ya zoezi la uchangiaji wa Madawati mashuleni.

Na Khadija Seif, Michuzi Tv
KLABU ya Rotary yakabidhi Madawati 200 kwa Shule ya Msingi Minanzini huku wadau wengine wakiombwa kuboresha miundombinu mbalimbali mashuleni ili kuwajengea uwezo wanafunzi kufanya vizuri Masomo yao.

Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 02,2023 Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule wakati wa kupokea Madawati hayo amesema Rais Dkt.Samia Suluhu ameendelea kuweka Mazingira mazuri kwa wawekezaji na wadau mbalimbali kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kusaidia na kutoa michango kwa jamii.

"Wadau wetu wa Rotary club Dar wametupatia Madawati 200 yenye thamani shilingi milioni 30 pamoja na vitabu kwa Shule ya Msingi Minanzini lakini wadau hawa wamekuwa wakiendelea na utaratibu wakufika shule mbalimbali mara ya mwisho walitembelea Shule ya Msingi Mwananyamala B na kugawa Madawati 100 yenye thamani ya Shilingi Milioni 13 na laki tano.

"Madawati niliyopokea Leo hii yataenda kuleta tija pamoja na kuleta chachu ya Maendeleo ya kufanya vizuri kwa wanafunzi hawa."

Pia ametoa rai kwa walimu na wazazi kuhakikisha wanafata taratibu na sheria ili kutoa adhabu zitakazowaimarisha na kuwajenga wanafunzi kuliko kutoa adhabu zitakazowaumiza na kuharibu saikolojia yao.

Nae Rais wa Klabu ya Rotary Nikita Aggarwal amesema wataendelea kugawa Madawati kwa shule zenye uhitaji zaidi kadri fedha zinavopatikana kutoka kwenye michango ya wanachama wa Rotary klabu na marafiki wa Rotary ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira rafiki kwa kusomea.

"Madawati tuliyotoa hadi sasa yamewanyanyua chini watoto zaidi ya 6,000 ambao walikuwa wanakaa chini wakiwa madarasani".

Hata hivyo Aggarwal ameeleza kuwa wataendelea na mradi wa kutoa Madawati ambapo unaenda sambamba na zoezi la upandaji wa miti ili kuhifadhi mazingira.

''Hivi sasa Mradi wetu huu umeshatoa zaidi ya Madawati 2,000 yenye thamani ya Shilingi Milioni 300 kwa shule mbalimbali.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Minzani amewapongeza Klabu hiyo na kuwaomba wasaidie shule zingine ili kuboresha miundombinu mbalimbali na kuweka Mazingira rafiki kwa wanafunzi mashuleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...