Na mwandishi wetu
WITO
umetolewa kwa watanzania, hususan wafanyakazi wanaotumia muda mwingi
kufanya kazi wakiwa wamekaa kufanya mazoezi, ili kuimarisha afya zao na
kujiepusha na magonjwa nyemelezi.
Wito huo umetolewa na Mkaguzi
wa Ndani wa Benki ya Biashara ya DCB, Bwana Samwel Mahendela wakati wa
mbio za mwaka huu za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon, zilizotimua
vumbi katika mji wa Moshi, Mkoani Kilimanjaro Leo.
Akiongoza
timu ya wafanyakazi 40 wa benki hiyo kushiriki mbio hizo mjini hapa,
Bwana Mahendela alisema, mbio hizi ni muhimu hasa kwa wafanyakazi wa
sekta ya mabenki kwani hutumia muda wao mwingi kuhudumia wateja wakiwa
kwenye viti.
“Kushiriki mbio kama hizi pamoja na mazoezi ya
viungo kwa ujumla vinaimarisha afya ya mwili na akili na kuongeza
ufanisi wa kazi, mara nyingi tunafanya kazi tukiwa tumekaa na pia
hatuna muda wa kutosha wa kufanya mazoezi.
“Natoa wito kwa
wafanyakazi wa sekta za mabenki pamoja na watanzania kuchangamkia mbio
za Kilimanjaro Marathon ili kuimarisha afya zao.
“ Natoa
pongezi pia kwa benki yetu pendwa ya DCB kwa kutuwezesha sisi
wafanyakazi wake kushiriki mbio hizi lakini pia kwa kuisapoti DCB
runners club, DCB tupo Imara tunasonga mbele.
Meneja Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya Biashara ya DCB, Samwel Mahendela ( katikati) akikimbia mbio za km 21.1 na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Picha nyingine ni baadhi ya wakimbiaji wa DCB wakishiriki mbio hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...