Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

Baraza la Madiwani la Kibaha Mji ,limepitisha bajeti ya Sh.bilioni 48.6 na kuridhia makadirio na Matumizi kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwa na ongezeko la bilioni 2,845,940,730 ukilinganisha na bajeti ya Sh. 45,809,511,506 ya Mwaka wa fedha 2022/2023.

Kambi Legeza Diwani wa Kata ya Visiga aliyewasilisha bajeti hiyo kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti ,Selina Msenga alisema kati ya fedha hizo,Sh. bilioni 6,563,628,000 ni Mapato ya ndani,Bilioni 41,161,858,000 ni ruzuku kutoka Serikali kuu na wafadhili mbalimbali huku Milioni 929,966,236 zikitoka kwenye vyanzo vingine ikiwemo Bima ya afya na Mchango wa Jamii.

Akifafanua matumizi ya fedha hizo Mhe.Legeza alieleza kuwa jumla ya fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 31,094,816,000 itatumika kulipa mishahara ya watumishi,milioni 824,226,000 ikitumika kwa matumizi ya kawaida na Miradi ya Maendeleo ikitumia kiasi cha Bilioni 9,242,816,000

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha ,Mussa Ndomba alisema kuwa bajeti ya Mwaka 2023/2024 imekuwa shirikishi kwani imeanza kuchakatwa kuanzia ngazi ya Mtaa na itatekeleza vipaumbele vya Wananchi ikiwemo Elimu,Afya,Maendeleo ya Jamii kwa kutoa Mikopo ya akina Mama,Vijana na wenye ulemavu.

Alitoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji ili kufikia malengo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...