Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu (kulia), wakiangalia wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed akisaini makubaliano yatakayowawezesha wateja wa benki hiyo kununua nyumba za NHC kwa mkopo kutoka benki hiyo. Ilikuwa ni wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Mkopo wa nyumba ulioboreshwa wa Absa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya mkopo wa nyumba ulioboreshwa wa Benki ya Absa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Ndabu Lilian Swere, akizungumza katika hafla hiyo jijini humo hivi karibuni.

Meneja Bidhaa za Mikopo wa Benki ya Absa Tanzania, Patricia Nguma akitoa maelezo kuhusu huduma za mikopo ya nyumba za Absa wakati wa hafla hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahudhuriaji katika hafla hiyo wakifurahishwa na hotuba ya mgeni rasmi, Waziri wa Ardhi, Dk. Angeline Mabula wakati akizindua hduma ya Mkopo wa nyumba ulioboreshwa wa Benki ya Absa uliofanyika pamoja ya utiaji saini makubaliano kati ya Absa na Shirika la Nyumba la Taifa kuwawezesha wateja wa benki hiyo kununua nyumba za NHC kwa mkopo. Uzinduzi ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...