CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)kimewahimiza wazazi na walezi katika Wilaya ya Manyoni mkoani Singid kuhakikisha wanawapeleka vijana wao katika Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) ili wapate ujuzi utakaowawezesha kujiajiri kuliko kukaa vijiweni kupiga soga na Kushawishiwa kwa maneno ya 'Komaeni'.


Akizungumza leo Februari 27,2023 akiwa mkoani Singida Katibu Mkuu wa CCM
Daniel Chongolo amesema Serikali inajenga VETA kila wilaya ili kuwapa vijana ujuzi utakaowawezesha kunufaika na fursa za kiuchumi zinazopatikana kwenye maeneo yao.

"Tusiache kupeleka vijana wetu kupata mafunzo ya ufundi, Vijana wamekuwa na dhana kwamba akiwa na shahada ya historia au Kiswahili hawezi kujifunza ufundi, siyo kweli. Tunajenga VETA kila mahali kwa ajili ya vijana wenu kujifunza ufundi ili kunufaika na fursa zinazopatikana," amesema Chongolo.

Katika hatua nyingine Serikali mkoani Singida imeunda timu ya Uchunguzi wa matukio ya mauaji na unyofoaji wa viungo vya maiti, ambayo yanadaiwa kujitokeza kwa siku za hivi karibuni hasa katika Wilaya ya Manyoni.

Akizungumza mbele ya Katibu Mkuu,Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema wameamua kuchukua hatua kukabiliana na matukio ya mauji ikiwa pamoja na kuunda timu Maalum ya kufuatilia matukio hayo

Surukamba ametoa maelezo hayo baada ya Chongolo kutaka maelezo ya kina kuhusu matukio hayo kutokana na kupokea malalamiko ya wananchi wakieleza kukithiri kwa matukio ya aina hiyo ya mauaji ya kikatili.

Serukamba amesema matukio hayo yanapata msukumo kutokana na Imani za kishirikiana."Ndugu Katibu Mkuu wetu, ni kweli kumekuwepo na aina hiyo ya mauaji na kisha maiti kuondolewa viungo, ambayo Chanzo chake hasa ni Imani potofu za kishirikina kwa hiyo tumeunda timu ya Watalaamu kwa ajili ya kufanya Uchunguzi ili kubaini hasa kiini chake" amesema Serukamba.

Kwa upande wake Chongolo akielezea kuhusiana na hilo, amesema CCM kimepewa jukumu la kuhakikisha inawalinda wananchi na kila aina ya uovu na kwamba ,imeandikwa kwenye Ilani yake yake ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025 katika Ukurasa wa 303.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Daniel Chongolo yupo mkoani Singida kwa ziara ya Siku 6 yenye lengo la Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, akiambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Haji Issa Gavu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wa shina namba 5, Manyoni ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, Manyoni mkoani Singida
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipitia taarifa ya shina namba 5 Kata ya Manyoni,walioketi pamoja nae ni Mwenyekiti wa Shina Bi. Fatma Juma (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Ndugu Martha Mlata (kulia) ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, Manyoni mkoani Singida.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Singida Ndugu Peter (kushoto) wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Solya iliyopo Tarafa ya Kilimatinde, Kata ya Solya, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Solya mkoani Singida.
 Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi (Gavu) akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Solya mkoani Singida.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida Mhandisi Msama Costatine Msama (kushoto) alipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara Itigi- Rugwa Wilayani Manyoni mkoani Singida kwa kiwango cha lami cha kilomita 25 kwa gharama ya shilingi bilioni 29.7





Baadhi ya Wanachi na Wana CCM wakiwa wamekusanyika wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo alipowasili eneo hilo kwa ajili ya kukagua mradi wa maji Kitinku Lusilile ambao utasaidia kuhudumia Wananchi 55,000 wa vijiji 11 vya kata nne za Wilaya hiyo.


Wananchi na wana CCM wakishangilia mara baada ya kuelezwa kuhusu mradi huo wa maji Kitinku Lusilile ambao utasaidia kuhudumia Wananchi 55,000 wa vijiji 11 vya kata nne za Wilaya hiyo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akishuhudia bomba la mradi wa maji Kitinku Lusilile ambao utasaidia kuhudumia Wananchi 55,000 wa vijiji 11 vya kata nne za Wilaya hiyo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na Usimamizi wa Mazingira Vijijini Singida (RUWASA) Mhandisi Lucas Said alipokuwa akimuelezea kuhusu kukamilika kwa mradi wa maji Kitinku Lusilile ambao utasaidia kuhudumia Wananchi 55,000 wa vijiji 11 vya kata nne za Wilaya hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...