Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo mwenyekiti kanzu akikabidhi msaada wa chakula kilo 400 kwa wazee wenye ulemavu wa kuona katika Kijiji cha Mwenge kata ya Mitumbati

Baadhi ya wazee wenye ulemavu wa kuona katika Kijiji cha Mwenge kata ya Mitumbati wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alipokuwa akitoa msaada huo.Na Fredy Mgunda, Nachingwea


MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ametoa msaada wa chakula kilo 400 kwa wazee wenye ulemavu wa kuona katika Kijiji cha Mwenge kata ya Mitumbati kutoka na kukabiliwa na uhaba wa chakula kwa wazee hao.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa ametoa msaada huo kufuatia ombi la wazee wenye ulemavu wa kuona kumuomba awasaidie chakula.

Alisema kuwa akiwa wananchi wa wilaya ya Nachingwea anapaswa kuchangia misaada pale inapowezekana hivyo aliguswa na wazee hao ndio maana akatafuta chakula hicho na kuwapelekea walemavu hao wa macho katika Kijiji cha Mwenge kata ya Mitumbati.

Moyo aliishukuru benki ya NMB kwa kuchangia msaada wa chakula kwa wazee wenye ulemavu wa kuona kwa kumuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo kusaidia chakula ambacho walikuwa na uhitaji nacho.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alimazia kwa kuwaomba wadau wengine kuwasaidia wazee wenye ulemavu wa kuona chakula na huduma nyingine kwa kila mtu ni mzee ajaye .

Kwa upande wao baadhi ya wazee wenye ulemavu wa kuona walimshukuru mkuu wa wilaya ya Nachingwea na benk ya NMB kwa msaada wa chakula kilo 400.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...