Na Jane Edward, Arusha
Wakurugenzi wa Halmshauri za Mkoa wa Arusha wametakiwa kubaini makundi au vikundi yanayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa zao ili kupata mafunzo kutoka Tume ya Ushindani (FCC) kwa lengo la kuongeza tija ikiwemo mnyororo wa thamani ,kwalengo la bidhaa kuwa na viwango kwenye ushindani wa soko.
Hayo yamejiri Jijini Arusha na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Musa Missaile wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uhamasishaji wa masuala ya ushindani na Udhibiti wa Bidhaa Bandia kwa wazalishaji Kanda ya Kaskazini.
Alisema endapo vikundi vinavyopewa mikopo na halmashauri vikipata mafunzo ya udhibiti wa ushindani wa kibiashara vitawezesha bidhaa zao kuingia katika masoko kutokana na ubora.
Aisha lengo la kutoa agizo hilo ni kukuza biasharana mnyororo wa thamani ikiwemo udhibiti wa bidhaa bandia na ukaguzi kwa walaji na wauzaji wa bidhaa mbalimbali.
"Wakurugenzi wa Halmshauri shirikianeni na FCC katika kuleta ushindani wa thamani za ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wanaopata mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri"
Kwa upande wake Mkuu wa FCC Kanda ya Kaskazini,Nonge Juma alisema mafunzo hayo kwa wafanyabiashara wa viwanda vidogo vya kati na vikubwa yanalengo la kuwezesha kuleta tija katika ushindani wa biashara wanazozalisha ikiwemo kudhibiti bidhaa bandia zisizizosajiliwa na kuleta athari kiuchumi.
Alisisitiza wafanyabiashara hao na wenye viwanda kuhakikisha wanazingatia maadili ya biashara ili kuhakikisha soko linabaki katika hali ya shindani .

.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...