Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imepokea ugeni kutoka Serikali ya India wenye lengo la kushirikiana katika ukuzaji wa teknolojia nchini.
Mkuu wa Msafara huo kutoka Taasisi ya Teknolojia India (IIT), Prof. Raghunathan Rengaswamy amesema Serikali ya India ni kinara katika teknolojia hivyo wanaangalia namna ambavyo watakuja kuwekeza hapa nchini.
Amesema kuwa Serikali hiyo inampango wa kuazisha Chuo cha Teknolojia (Indian Institute of Technology) nchini Tanzania hivyo wapo katika kuangalia vyuo mwenza katika teknolojia nchini.
“Timu hii tutakutana nayo tena Februari 17 mwaka huu na timu ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ili kwa pamoja tuangalie rasimu ya makuballiano (MOU) ili tuone tunakwendaje," amesema Rengaswamy.
Kwa upande wake Naibu Balozi wa India nchini, Manoj Verma amesema Serikali ya India imejizatiti kufanya kazi na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha pamoja na mambo mengine lengo la kuanzia Chuo nchini Tanzania linafanikiwa.
Naye Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Prof. Preksedis Ndomba amesema DIT imejipanga kuwa taasisi kinara katika masuala ya teknolojia katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii na kwamba taasisi hiyo ni taasisi sahii kwa serikali ya India kushirikiana.
"Ni fahari kubwa kupokea ugeni huu ambao unalenga kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma hapa nchini, tunashukuru sio tu kwa kuja DIT bali nia yenu katika kuhakikisha ushirikiano kati ya India na Tanzania unaimarika," amesema
Naibu Balozi wa India nchini, Manoj Verma akitoa zawadi kwa Taasisi ya DIT mara baada ya mazungumzo ya kuja kuwekeza hapa chini.
Naibu Balozi wa India nchini, Manoj Verma akitoa ufafanuzi kuhusiana na Chuo cha Teknolojia cha India wakati walipotembelea Taasisi ya DIT jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya ujumbe wa serikali ya India wakisikiliza ufafanuzi wa Taasisi ya DIT waipotembelea kwaajili ya kuangalia namna ya kushirikiana katika ukuzaji wa Teknolojia nchini.
Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam (DIT), Preksedis Ndomba akizungumza na Ujumbe kutoka Serikali ya India jijini Dar Es Salaam leo wakati walipokuja kuangalia mazingira ya uwekezaji hapa nchini.
Naibu Balozi wa India nchini, Manoj Verma akitoa ufafanuzi kuhusiana na Chuo cha Teknolojia cha India wakati walipotembelea Taasisi ya DIT jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya ujumbe wa serikali ya India wakisikiliza ufafanuzi wa Taasisi ya DIT waipotembelea kwaajili ya kuangalia namna ya kushirikiana katika ukuzaji wa Teknolojia nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...