Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema kuwa itaendelea kushirikiana na kampuni changa za TEHAMA, kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya ufanyaji kazi pamoja na kuwafungulia masoko.

Kuwezesha Masoko kwa kampuni changa za TEHAMA itasidia kuongeza uchumi wa Taifa na kuongeza ajira kwa vijana ambao watapata fursa ya kuonesha bunifu zao katika sekta ya Teknolojia.
Hayo yameelezwa leo Februari 14,2023 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt.Jimmy Yonazi wakati wa hafla ya utiaji saini kati ya Wizara ya habari , mawasliano na Taknologia ya habari na Tanzania Startup's (TSA) Association (TSA) , kwa ajili ya uanzishwaji na uimarishaji wa Miongozo mbalimbali inayosimamia bunifu na kampuni changa nchini.

Yonazi amesema kuwa Wizara hiyo ina sera na sheria rafiki zinazowezesha makapuni machanga kufanya kazi zao kwa uhuru hivyo ujio wa (TSA) utasaidia kupeleka uchumi wa makampuni machanga mbele ndani na nje ya nchi.
"Serikali ipo tayari kushirikiana na kampuni hizi changa na lengo letu sio tu kwamba tunaongeza uchumi kwa makampuni na taifa ila lengo letu ni kulikomboa bara la Afrika kwa upande wa TEHAMA kwani kwa sasa soko la dunia limehamia upande wa digitali,"amesema Dkt.Yonazi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Startups Association (TSA) Zahoro Muhaji amesema kuwa bara la Afrika linakabiliwa na changamoto kubwa ya ajira hivyo TSA imeona hilo na kwa sasa inaendelea kufungua fursa za ajira kupitia TEHAMA.

"Tumeanza safari nzuri ya kufanya kazi na Serikali kupitia Wizara hii Mama ya mawasiliano na ahadi yetu kubwa ni ushirikiano wa kutosha wenye tija kwa taifa letu na jamii kwa ujumla,"amesema Zahoro.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...