KIKOSI cha Ruvu Shooting FC Kinatarajia kuondoka Mkoani Morogoro siku ya February 15, 2023 kuelekea Mkoani Geita kwenda kutupa karata yake ya 23 katika msimu wa ligi kuu ya NBC 2023 dhidi ya wenyeji wao Geita Gold FC, mchezo unaotarajiwa kutimua vumbi February 17, 2023, katika dimba la Nyankumbu.

Akizungumza na Michuzi TV Mwalimu Mkuu wa kikosi hicho Mbwana Makata, ametamba kuondoka na alama tatu muhimu ugenini ili aweze kuinusuru timu yake kukumbwa na kadhia ya kushuka daraja.

Aidha mwalimu Makata amesema jumla ya wachezaji 22 watasafiri na timu kuelekea mkoani Geita kwa lengo la kutimiza jukumu hilo, huku wengine watasalia kambani na kuendelea kujitayarisha kwa mapambano dhidi ya michezo iliyosalia mbele yao.

Ruvu Shooting FC inaenda kuwavaa Geita Golg wakiwa katika nafasi ya pili kutoka mwisho, huku wakiwa na kumbu kumbu ya kushinda mchezo wao uliopita waliocheza katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo waliibuka kifua mbele dhidi ya KMC kwa kuwachalanga mabao 2 – 1.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...