Klabu ya KMC FC leo imepokea basi jipya lenye thamani ya shilingi milioni 450 ambalo limetolewa na Benki ya NBC kwa makubaliano ya mkopo wa mwaka mmoja kwa lengo la kurahisisha usafiri kwa wachezaji.
Basi
hilo limekabidhiwa mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amosi
Makala, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambuli, Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge, Mkurugenzi Hanifa Suleiman
Hamza pamoja na Makamu Mwenyekiti wa KMC FC Mhe. Rehema Mandingo.
Akizungumza
wakati wa kukabizi gari hilo la kisasa linaloweza kubeba watu 58 Mhe.
Makala ameipongeza Timu ya KMC FC kwakuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha kwamba inawajali wachezaji wake na hivyo kuwapatia huduma
nzuri ya usafiri.
"
Niwapongeze sana KMC FC kwakuona fursa hiii kutoka Benki ya NBC ambao ni
wazamini wakuu wa Ligi yetu, Timu nyingine ziige na kuacha visingizo
vya magari kuwa yapo gereji, KMC FC imeonesha ukubwa wao na mazingatio
ya malengo waliyokuwa nayo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambuli amesema
" Tunafahamu wote faida ya michezo, leo tumepokea basi hili na hivyo
ninampongeza Mkurugenzi, Meya kwa kufanikisha hili na hivyo kupunguza
gharama ya uendeshaji wa usafirishaji wa timu.
Mtambuli ameishukuru
pia Banki ya NBC kwakujitoa kwenye ligi lakini pia kushuka hadi kwenye
Timu ya KMC FC kwa kukubali kutoa gari wenye mkopo nafuu na kuahidi
kulitunza ili liweze kutumika vizuri sambamba na kusimamia mkopo huo
ili uweze kurudi kwa wakati na hivyo kuendelea kuwekeza zaidi katika
sekta hiyo muhimu ya michezo.
Kwa upande wake Mstahiki Meya , Mhe.
Songoro akipokea basi hilo amesema kuwa kama Manispaa ya Kinondoni
imejipanga kwa kuweka kwenye bajeti malipo ya mkopo huo kwa kipindi cha
mwaka mmoja na kufanikisha kwa ufanisi mkubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...