Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na uongozi wake kwa kutekeleza kajukumu yao kwa mafanikio makubwa.

Mhe. Hemed ametoa Pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Bodi hiyo Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.

Amesema ni muda mchache tokea kuanzishwa kwa Wakala huo ambapo wameanza kutekeleza dhamira ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya kuwawezesha wanchi kupata mitaji na kutoa fursa za kukuza uchumi na kupunguza changamaoto zinazoikabili jamii.

Amesema ni vyema kwa wakala huo kuanzisha mifumo ya kieletroniki katika shughuli za uendeshaji ili kuweza kutoa huduma bora Zaidi na gharama nafuu kwa wananchi.

Aidha Mhe. Hemed ameridhishwa na utendaji kazi wa wakala kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na Sekta binafsi na washirika wa maendeleo ndani na nje ya nchi katika utafutaji na upatikanaji wa rasilimali fedha.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Ndg. Juma Amour Mohammed amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa baada ya kuchaguliwa kwa Bodi hiyo wameweza kutayarisha muundo wa taasisi pamoja na kuandaa mpango mkakati na kuratibu upatikanaji wa rasilimali fedha.

Aidha ameeleza kuwa Bodi inaendelea na mazungumzo na wadau mbali mbali wa Maendeleo kwa lengo la kukuza sekta ya Uwezeshaji nchini.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa wakala wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi Ndg. Juma Burhan amesema kuwa jumla ya wananchi 17,665 wamenufaika na fedha za uwezeshaji kati ya hao 8686 kutoka unguja wakiwemo wanaume 3311 na wanawake 5375 aidha kwa upande wa Pemba jumla ya wananchi 8979 wamenufaika wakiwemo wanaume 3425 na wanawake 5554.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na uongozi wake waliofika kijitambulisha Ofisini kwake Vuga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...