Mawakala Utalii wamiminika nchini

MAWAKALA wa Utalii wameanza kumiminika nchini ili kuangalia vivutio vya Utalii hapa nchini na kwenda kuvitangaza nchini mwao.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Eliamani Sedoyeka jana aliongoza mapokezi ya Mawakala hao kutoka katika masoko ya kimkakati katika nchi tofauti.

Nchi walizotoka Mawakala hao ni Marekani, Canada, Mexico, Ubelgiji na Brazil.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea Mawakala hao, Prof. Sedoyeka amesema "Leo tumeanzisha Mega Trip ambayo kwa kawaida Wizara kupitia Bodi ya Utalii ( TTB) uandaa safari kama hizi ambazo uwaleta waongoza Utalii, Waandishi wa Habari na wadau wakuu wa utalii wa kimkakati ili waje Tanzania kuangalia maeneo yetu mbali mbali ya vivutio".

Sedoyeka amesema watalii wanavyokuja nchini uletwa na makampuni ambayo tayari kama nchi imeshawajengea uwezo Mawakala wa nchi hizo juu ya vivutio vilivyopo nchini.

"Ziara hii inakuja baada ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa na mashirikino mazuri na kampuni ya Ndege ya Qatar na pia ni muendelezo wa matunda ya Royal Tour iliyoongozwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. " Amesema Sedoyeka

Amesema, Tanzania imeingia makubaliano ya kimkakati kuanzisha mahusiano ya kibiashara ili kuwatangazia duniani kuwa Tanzania kuna vivutio vya aina gani, mahusiano ya kimkakati ili kumtengenezea mtiririko wa wageni.

Amesema, kufunguka kwa masoko ya kimataifa yanasaidia kukua kwa uchumi wa nchi na kuongezeka kwa pato la taifa. Wafanyabiashara wanapata fedha.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...