NA STEPHANO MANGO, MBINGA

WANANCHI wa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini Jonas Mbunda kwa kitendo chake cha kupigania mpango wa utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Mbinga Mjini -Luwaita kwa kiwango cha Lami ( Mradi wa Agriconnect) ili kuweza kuwarahisishia wananchi katika sekta ya usafirishaji

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema kuwa wanaungana na Mbunge wao kuiomba Serikali kuharakisha mradi huo ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi katika kuharakisha maendeleo

“Tunaiomba Serikali kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ili kutatua changamoto za usafiri wa abiria na mizigo hususani katika kipindi cha masika ambako kumekuwa na kero kubwa sana kwa wananchi hali ambayo inasababisha uchumi kuzorota” Alisema Dotto Ponera

Alieleza kuwa barabara hiyo ni ya kimkakati hivyo Serikali inatakiwa kuipa kipaumbele sana kwa maslahi ya wananchi ambao wamekuwa wakiitegemea sana barabara hiyo kwa shughuli zao za uzalishaji mali

Hivyo kitendo cha Mbunge wetu Jonas Mbunda akiwa katika kikao cha Bunge la 12 Mkutano wa 10 kuihoji Serikali kuhusu mradi huo kimeendelea kutupa faraja na tunampongeza sana kwa kuendelea kuwatetea wananchi wake

Mbunge huyo aliuliza swali kwa Waziri wa OR- TAMISEMI kuhusu mpango wa utekelezaji wa mradi wa Agriconnect ambao unalenga kujenga barabara za Lami kuunganisha mashamba/eneo la uzalishaji na soko/ghala ambayo kwa Jimbo la Mbinga Mjini mradi huo unatarajiwa kujenga barabara ya Luwaita- Mbinga Mjini yenye urefu wa 15 Kilometa.

Akijibu swali hilo David Silinde, Naibu Waziri TAMISEMI alieleza kwamba Agriconnect ni program inayofadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) inayolenga kujenga barabara za kusafirisha mazao kutoka mashambani/maeneo ya uzalishaji kwenda sokoni, Viwandani na kwenye maghala. Utekelezaji wake unafanyika kwa awamu tatu na barabara ya Luwaita ipo katika awamu ya tatu ambayo utekelezaji wake utaanza mwaka wa Fedha 2023/2024.

Aidha, hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo zinafanyika ikiwemo uainishaji,uhakiki na upangaji wa vipaumbele vya barabara katika mikoa ya Ruvuma, Njombe,Iringa, Mbeya, Katavi na Songwe.

Hata hivyo Mbunge aliishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwaajili ya Ujenzi wa barabara hiyo, Pia aliomba utekelezaji wa mradi huo uharakishwe ili wananchi wa Kata za pembezoni ikiwemo Kata ya Luwaita wanaotumia barabara hiyo waweze kurahisishiwa usafirishaji wa mazao yao.

Naye Naibu Waziri alimhakikishia Mbunge Mbunda kwamba utekelezaji huo utafanyika kwa wakati kwani barabara ambazo zipo kwenye awamu ya kwanza na ya pili utekelezaji unaendelea.

Naye Betram Kapinga Mkazi wa Jimbo hilo alisema kuwa barabara hiyo ina manufaa makubwa sana kwa jamii kwani huchangia pakubwa katika maendeleo ya nchi. Raia wa Sehemu kulikojengwa barabara hupata urahisi katika utekelezaji wa shughuli zao. Mathalan, mfanyabiashara anayetaka kusafirisha mizigo au bidhaa zake, hurahisishiwa na raia hunufaika kwa kununua kwa bei nafuu.

Kapinga alisema kuwa wananchi wa Jimbo hilo wataendelea kumpa ushirikiano Mbunge wao ili aweze lutekeleza vyema Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka wa 2020/2025 kwa maslahi ya wananchi ambao ndio wapiga kura
Jonas Mbunda akizungumza kwenye kikao cha Maendeleo Wilaya ya Mbinga, Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo Aziza Mangosongo, wakwanza kulia ni Mbunge wa Mbinga Vijijini Benaya Kapinga

Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini Jonas Mbunda aliyevaa shati jeupe, wanne toka kushoto ni Katibu wa Ccm Wilaya ya Mbinga Marry Mwenyishingole wakizungumza na Waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara ya kusikiliza kero za w

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...