Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKAZI  wa Sumbawanga mkoani Rukwa, Japhet Msangawale ameibuka mshindi wa Supa Jackpot ya Kampuni hiyo baada ya kupata ubashiri wa jumla ya mechi 13/13 katika ubashiri wake na kupata kitita cha Tsh. Milioni 248,672,790.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya SportPesa, Tarimba Abbas amempongeza Japhet baada ya kuibuka kuwa mshindi wa Supa Jackpot hiyo siku ya Jumapili, usiku wa Februari 12, 2023 majira ya saa tano usiku.

“Kama ilivyokuwa dhamira yetu tangu awali ya kuwawezesha Watanzania ambao wanabashiri na Kampuni yetu ya SportPesa, leo ninayo furaha ya dhati kumtambulisha na pia kumkabidhi mfano wa hundi ya pesa yake, Japhet Msangawale Mamboleo ambayo ameshinda siku ya Jumapili usiku,” amesema Tarimba.

“Mshindi huyu ni kijana mdogo wa miaka 25, ambaye kwa miaka takriban mitatu na zaidi alikuwa anajaribu kutimiza ndoto zake, na leo hii, ndoto hiyo si ya kusadikika tena, bali imekuwa ndoto ya kweli, ameeleza Tarimba.

Kwa upande wake, Mshindi huyo, Japhet ameishukuru SportPesa kwa ushindi wake wa kiasi kikubwa cha fedha ambacho pengine isingekuwa rahisi kwake kukipata katika mazingira yake ya kawaida.

‘’Nachukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kuwashukuru SportPesa kwa kunileta Dar es Salaam, na kwa mara ya kwanza nimepanda Ndege, kitu ambacho nilikuwa sitegemei katika maisha yangu,” amesema Japhet.

“Mwanzoni nilikuwa siamini kama nitaipata pesa hii, lakini baada kushinda nilipata ujumbe wa kunipongeza kwa ushindi wa Supa Jackpot na baadae usiku uleule nilipigiwa simu na mtoa huduma kwa wateja ambaye alinitaarifu juu ya ushindi wangu na kuniambia nitapigiwa simu ili nipewe utaratibu wa namna ya kuja Dar es Salaam, kuhakikiwa na kuthibitishwa na kisha kulipwa fedha zangu,” ameeleza Japhet.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...