Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (MNEC) kupitia Wazazi Hamoud Jumaa amefika kitongoji cha Matuga kata ya Kawawa,kuwafariji wahanga waliokumbwa na Zoezi la bomoabomoa ya makazi yao ambapo amewapatia vyakula.
Amewafariji wahanga kwa kuwapatia Unga, Sukari, Maharage, Pesa taslimu kwaajili ya vyoo vya dharura vya wanawake na wanaume.
Jumaa ameeleza ,anatambua wapo kwenye wakati mgumu na kuwaomba wahanga wawe na subira kwani Serikali na Chama Viko vinalifuatilia suala hilo kwa ukaribu na haki zitapatikana.
Amesema kwakuwa jambo hilo lipo katika mchakato wa kisheria ni vyema kuisubiria serikal itakuja na majibu sahihi.
Kitongoji cha Matuga kimekumbwa na bomoabomoa ya nyumba takriban 152 baada ya Maamuzi ya baraza la ardhi wilaya kuamuru eneo kurudi kwa mmiliki KADRI ambae wakazi hao na upande wa Zegereni kuvamia eneo la mmiliki huyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...