TAASISI binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo(PASS)imezindua kampeni ya Kijanisha maisha kwa wadau wake wa ndani ili kuelewa na kufahamu dhana hiyo inayotokana na mpango kazi wa kuhimiza kijani shirikishi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust,Yohane Kaduma alisema dhumuni kuu la uzinduzi huo ni kukuza mageuzi ya biashara ya kilimo katika sekta ya kilimo.
“Kijanisha maisha ni kampeni mwamvuli yenye wito wa kuhamasisha wadau wote wa kilimo biashara kufuata kanuni za uzalishaji zinazofuata ukuaji wa kijani shirikishi ambazo ni pamoja na matumizi bora ya maliasili, ulinzi wa makazi unaojumuisha bioanuwai na mifumo ikolojia yake,uzalishaji kidogo wa hewa ya kaboni ili kupunguza kiwango cha kaboni, ushirikishwaji wa wanawake na vijana, usawa na haki ya kijamii, uvumbuzi na uundaji wa ajira ya kijani shirikishi.”alisema Kiduma
Alisema Kilimo kinacho zingatia ukuaji wakijani shirikishi kitasaidia wadau wa kilimo biashara kutoka sekta ya uvuvi, ufugaji, na misitu kupata mikopo kutoka taasisi za fedha kupitia mfumo wa udhamini wa mikopo wa PASS ambapo wajasiliamalihao wana nafasi ya kupata dhamana ya mikopo ya hadi 80%.
Kaduma anaongeza kuwa Katika dunia ya sasa mabadiliko ya hali ya hewa ni ajenda kuu ya kimataifa,ambapo PASS Kama mawakala katika kufanya mabadiliko kupitia sekta ya kilimo tunahitaji kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wote muhimu wakiwemo watoa huduma za Kifedha, asasi za kiraia, mashirika ya mazingira,na
wafadhili wa mashirika mengine wa ili kufikia lengo moja la mabadiliko ya kilimo biashara kwa kuzingatia ukuaji wa kijani shirikishi na utachochea ukuaji wa kilimo endelevu.
Akielezea namna wakulima walivyo katika nafasi nzuri ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia kampeni ya Kijanisha maisha. Kaduma alisema inawezekana baada ya miaka michache tukawa katika kiwango kizuri kiuchumi kwa sababu Kijanisha maisha itachochea kilimo endelevu ambacho kitakuwa na manufaa kwa biashara ya kilimo nchini.
Tangu kuanzishwa kwa Kijani shirikishi , mpaka Desemba 2022, jumla ya miradi ipatayo 66, 077zilinufaika na dhamana kutoka PASS, zikiwafikia takribani wanufaika 3,427,960 na kutengeneza ajira zipatazo 2,712,048.
PASS inapatikana nchi nzima kupitia ofisi zake za kanda zilizopo kama ifuatavyo, Kanda ya Ziwa, Mwanza; Kanda ya kati na mashariki, Morogoro; kanda ya kusini, Ruvuma; kanda yakaskazini, Arusha; Kanda ya magharibi, Tabora; Kanda ya nyanda za juu kusini, Mbeya namakao makuu yake, Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...