MSITU wa Hifadhi wa Taifa wa mazingira asilia Mwambesi uliopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ulianzishwa mwaka 1956 na ulipandishwa hadhi kuwa msitu wa Taifa katika kipindi cha mwaka 2017/2018.

Meneja wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilayani Tunduru Denis Mwangama anasema msitu huo umepandishwa hadhi ili kuongeza uhifadhi zaidi kutokana na kuwa na utajiri wa viumbe vya kipekee duniani wakiwemo wanyama,ndege na mimea.

Anawataja wanyama waliopo katika msitu huo ambao upo kando kando mwa Mto Ruvuma kuwa ni simba, tembo, chuo,kuro,jamii za nyani,jamii za swala,nyati na wanyama wengine.

Mwangama anasema Katika msitu wa Mwambesi kuna jamii ya ndege maarufu duniani anayeitwa Pentiole ambaye utafiti uliofanywa na PALMS Foundation mwaka 2015 umebaini kuwa ndege huyo amehamia kutoka nchi ya Madagaska baada ya mazingira aliyokuwa anaishi kuharibiwa na shughuli za kibinadamu.

Kwa mujibu wa Mwangama, ndege huyo ana tabia ya kuzamia samaki kutoka majini na kwamba ndege hao wanapenda kuishi kwenye maporomoko ya Mto Ruvuma yanayoitwa sunda ambayo yapo ndani ya hifadhi hiyo.

“Tanzania tuna bahati katika msitu wetu tuna ndege Pentiole ambaye amekuwa akiishi ukingoni mwa maporomoko ya maji yajulikanayo kama Sunda Water falls’’,anasisitiza.

Kwa mujibu wa Mwangama Ndege huyu huogolea kwankufuata mdondoko wa mawimbi ya maji kwenye maporomoko hayo akitatafuta mawindo yake ya samaki ambacho ndicho chakula chake pekee.

Licha ya ndege huyo Mwangama anayataja maporomoko ya Sunda kuwa ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika hifadhi ya Mwambesi na kwamba maporomoko hayo yalitumika wakati wa vita ya Majimaji kati ya mwaka 1905 hadi 1907 ili kujificha kwenye mapango kwa juu.

Anasema Mto huo ndio uliokuwa ukitumika kwenye vita vya Majimaji ambapo watu wa makabila au ukanda wa kusini hususani Wangoni walitumia maji yake katika kuzimia silaha za moto chini ya uongozi wa Kinjeketile Ngwale.

Kulingana na Mwangama, eneo hilo pia linaaminika Wajerumani walitumia kama njia kubwa wakitokea Msumbiji katika biashara ya meno ya Tembo na kwamba Waarabu walipita pembezoni mwa mto huo kuwapitishia watumwa.

Hata hivyo anasema awali kabla ya serikali kuamua msitu huo kuwa Msitu wa hifadhi,kulikuwa na vitalu vya uwindaji wa kitalii ambapo ndani ya msitu kulikuwa na kambi ya wawindaji iliyoitwa Big Game iliyoendeshwa na Kampuni ya uwindaji iliyoitwa Tandara Hunting Safaris.

Kulingana na Meneja huyo,msitu huo una ukubwa wa zaidi ya hekta 112,000 na kwamba mtalii akiwa katika msitu wa Mwambesi anaweza kufanya utalii wa kuteleza kwenye mitumbwi katika mto Ruvuma.

Deborah Mwakanosya ni Meneja wa Msitu anasema Mwambesi ni msitu wa asili wa pili kwa ukubwa kwa Tanzania ukiongozwa na msitu wa Kilombero mkoani Morogoro.

Anasema msitu huo ambao umezungukwa na mto Ruvuma, umesheheni baianowai mbalimbali za mimea adimu duniani ikiwemo miti aina ya mipozipozi ambayo ina tabia ya kudondosha maji inapatikana sehemu chache duniani ukiwemo msitu wa Mwambesi.

Mwambesi ni moja kati ya Misitu mikubwa ya Hifadhi za Mazingira Asilia tulionayo wenye utajiri mwingi wa flora na fauna zakutosha.

Msitu wa Mwambesi unahifadhiwa kisheria chini ya uangalizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwa kushirikina na Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Kusini.

mapomoroko ya Sunda katika Mto Ruvuma  ndani ya hifadhi ya Mwambsi ambako ndege huyo anapenda kuishi kwa kula samaki ambacho ndicho chakula chake kikuuu

 Meneja wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Wilaya ya Tunduru Denis Mwangama
ndege jamii ya Pentiole ambaye utafiti umebani amehamia katika nkatika hifadhi ya Taifa ya Mazingira asilia Mwambesi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kutoka nchini Madagasca
fukwe za Mto Ruvuma ndani ya hifadhi ya Mwambesi moja ya maeneo ya kuvutia watalii wanaotembelea hifadhi hiyo inayopakana na nchi ya Msumbiji
baadhi ya watalii wa nje ya nchi wakiwasili katika hifadhi ya Taifa ya mazingira asilia Mwambesi wilayani Tunduru


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...