Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Pilsner Lager imefanya droo ya kwanza ya promosheni yake pendwa ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’ kubainisha washindi wa kwanza wa promosheni hiyo ambayo ni maalumu kwa wateja wa bia hiyo wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini.

Kupitia promosheni hiyo inayofanyika kwa muda wa wiki 8, wateja wa bia ya Pilsner watajishindia zawadi mbalimbali zikiwemo, televisheni, simu janja, pikipiki na zawadi ya mwisho ya gari. Droo iiliyofanyika jana, walipatikana washindi 7 kutoka kanda zote tatu, ambapo mshindi mmoja kutoka kanda ya Ziwa alishinda pikipiki, wengine watatu kutoka kanda zote tatu walishinda simu janja na wengine watatu walishinda televisheni. Washindi hao wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao tarehe 18 mwezi huu.

Washindi walioshinda simu janja ni Agatha Mvwango, Eli Elias na Hassan Joel; waliojishindia television za kisasa ni Justine Mwaipaja, Neema Abdallah na Selina Panga. Na mshindi wa bodaboda ni Neema Mathias kutoka kanda ya Ziwa.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Meneja wa bia ya Pilsner, Wankyo Marando alisema, droo hiyo ni mwanzo tu wa promosheni ya ‘Kapu la Wana’, akitoa wito kwa wateja wa bia ya Pilsner mikoa ya kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini kuendelea kushiriki kwenye promosheni hiyo kwani zawadi ni nyingi.

“Kupitia promosheni hii tunawazawadia wateja wetu wachapa kazi, na zawadi zipo nyingi sana hivyo nawatia moyo wateja wetu wa mikoa ya hizi kanda tatu, yani kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini waendelee kununua bia ya Pilsner, wapate kadi ya kukwangua, wakipata namba wataituma kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa namba 15320 baaada ya hapo watapokea ujumbe mfupi kudhibitisha ushiriki,“ alisema Marando.

Kwa upande wake, Muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania, Salim Mgafi aliwapongeza washindi wa droo hiyo ya kwanza kwa njia ya simu, na pia alipongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kufanya promosheni kwa kufuata kanuni na taratibu za bodi ya Michezo ya kubahatisha.

Hii ni mara ya pili bia ya Pilsner imekuja na promosheni hii ya ‘Kapu la Wana’ na imetenga zaidi ya Tsh. 36 milioni kwa washindi 22 wa kampeni hiyo.


 Menaja wa bia ya Pilsner, Wankyo Marando (Kulia) kutoka kiwanda cha bia cha Serengeti, akizungumza kwa njia ya mtandao na washindi wa droo ya kwanza wa promosheni ya bia hiyo ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’, iliyofanyika Dar es Salaam jana ambapo wateja saba wa bia ya Pilsner walijishindia televisheni za kisasa, simu janja na pikipiki moja. Kushoto ni muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Salim Mgafi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...