Na.Vero Ignatus,Arusha

Waziri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama (Mb) ameagiza Taasisi zote za umma ziwajibike kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na kama kuna mahali hawatumii wajitathmini,ili kupunguza urudufu wa uhitaji wa kila Taasisi ya Umma kuwa na mfumo wake.

Mhagama ameyasema hayo kwakati wa kufunga kikao kazi cha tu cha Serikali Mtandao Jijini Arusha, kuwa wapo wataalam wengi wanaotumia huduma za Kidigitali ambapo amewataka kuwa Wazalendo kwa Taifa sambamba na kuwataka kwenda kufanya thamini kwenye utendaji wao.

"Kuna baadhi ya wataalam wanaotumia huduma hizi za kidigitali kwa kunyofoa baadhi ya vitu kwenye mfumo mkongo wa Taifa, lakini hawana uzalendo kwa Taifa,ukishaambiwa mtandao upo chini ujue ukiona manyoya ujue ishaliwa
Watumishi wa umma tuongozwe na uzalendo kwa taifa ketu,nendeni mkafanye tathmini katika utendaji wetu" alisema Mhagama

Mhagama ameziaagiza Taasisi za Umma/Serikali kutekeleza maazimio yote yalioyopitishwa 12 kwenye kikao kazi cha siku 3 cha Serikali Mtandao (eGA)huku akiwataka kwenda kuyatumia kama kichocheo kikubwa cha kujenga ufanisi yatakayoendana na mabadiliko ya kasi ya teknolojia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa EGa Mhamdisi Benedict Ndomba alisema kuwa Kikao kazi hicho kimekuwa cha manufaa makubwa kwani wameweza kukaa na kujadiliana kwa pamoja namna ya kuweka mikakati na yakimkakakati namna ya kutatua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa ambapo washiriki 1624 waliweza kuhudhuria

Aidha amesema wamepokea maagizo ya mhe. waziri na kuahidi kwenda kuyatendea kazi sambamba lile la Taasisi idara na vitengo kujitahidi kutenga bajeti ya mafunzo pamoja na kuhakiiisha kuwa mafunzo hayo yanafanyika na haswa mifumo ya kukusanya mapato ya serikali

Wametoa ahadi kwamba wanakwenda kuhuisha tovuti zao na kuhakikisha kuwa taarifa zao kwmaba ni sahihi na kuhakikisha wanakwenda kufanya kazi kidigitali pampja na vikaonvyote vyankisheria vinakwenda kutekelezwa kidigitali

Katibu wa Viziwi tawi la Mkoa Pwani Suleiman Zalala (Chavita)aliyepata mualiko katika kikaokazi hicho cha siku tatu ameishukuru Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kuwashirikisha katika kikao kazi hicho na wamewaomba taasisi nyingine kutowasahau katika shughuli zao za kila siku

Mamlaka ya Serikali Mtandao ni taasisi iliyoanziahwa kwa sheria ya serikali Mtandao Na 10 mwaka 2019,ikiwa na majukumu ya kuratibu,kusimamiana na kukuza jitihada za serikali ,pamoja na kusmamia uzingaiaji wa sera,sheria,kauni naviwango, aambapo inaendeleza afua za wakala ya Serikali Mtandao iliyoundwa Aprili 2012 kwa sheria ya Wakala za serikali no.30 sura ya 245 ya mwaka 1997.

Kabla ya kuanzishwa kwa Wakala y Serikali Mtandao,matumizi ya TEHAMA serikalini yalikuwa yanaratibiwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti yaa utumishi wa Umma na Utawala Bora chini ya Idara ya Usimamizi wa Mifumo (DMIS)ambayo kwa sasa ni Idara ya Huduma za TEHAMA Serikalini (DICTS)

Aidha Mamlaka hiyo inaongozwa na misingi mikuu sita ambayo inaekekeza kuhusu tabia na mwenendo wa watumishi wake kwa ngazi zote ambayo ni: Uadilifu,Ubunifu,Kuthamini wateja,Ushirikiano pamoja na weledi.

Waziri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama (Mb)akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi cha siku tatu vha serikali Matandao Jijini Arusha


Pichani ni wajumbe wa kikao kazi cha tatu cha Serikali Mtandao kikiwa kinahitimishwa na Mhe.Mhagama kilichofanyika katika ukimbi wa kimataifa wa AICC

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...