Na Mwandishi Maalumu.


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panelof Elders, POE) ameongoza Ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatilia Utekelezaji wa Makubaliano ya Amani nchini Lesotho katika ziara nchini humo tarehe 08 – 11 Februari 2023.

 

Ziara ya Kamati hiyo ya Uangalizi ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Mkutano wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika Kinshasha, DRC mwezi Agosti 2022 ambapo walilielekeza Baraza hilo la Wazee la SADC kufuatilia kwa karibu jitihada za usuluhishi wa migogoro inayoendelea kwa muda mrefu katika Falme za Lesotho na Eswatini.

 

Rais Mstaafu Kikwete ameongozana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Mauritius,

Paramasivum Vyapoory, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wazee 

amepata wasaa wa kukutana na Mtukufu Motlotlehi Letsie III, Mfalme wa Lesotho, viongozi wakuu wa Serikali ya Lesotho pamoja na wadau wengine muhimu katika mgogoro huo.

 

Kamati pia imepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Lesotho ambaye ndiye Mkuu wa Serikali, Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Haki, Sheria na Masuala ya Bunge, Spika wa Bunge, Makamu Rais wa Seneti, Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Mabadiliko, Viongozi wa Vyama vya Siasa vya Upinzani vilivyo Bungeni, Vyama vya Siasa vilivyo nje ya Bunge, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Askofu Mkuu wa Baraza la Kanisa la

Kikristu nchini Lesotho pamoja na Mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Marekani, Uingereza, AfrikaKusini na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa.

 

Katika mikutano yote iliyofanyika, Kamati hiyo imesikiliza kwa kina maoni ya wadau hao wote kuhusu namna bora zaidi ya kuweza kuendeleza kazi nzuri ambayo tayari imeshafanyika katika kupata suluhu ya kudumu ya mgogoro uliopo nchini humo. Kamati hiyo inaripoti kwa Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika) ambaye kwa sasa ni Hage Geingob,Rais wa Namibia.







Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akiwa na Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Makamu wa Rais Mstaafu wa Mauritius Mhe. Paramasivum Pillay Vyapoory Pamoja na Ujumbe wa Seneti ya Lesoth alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.





Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akikutana na Mabalozi wa Uingereza na wa Umoja wa Ulaya alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akikutana viongozi wa Tume ya Taifa ya Mabadiliko ya Lesotho alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.





Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akiwa na kikao na Mwanasheria Mkuu wa Lesotho Mhe. Rapelang Motsieloa alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.




Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akikutana wawakilishi wa Asasi za kiraia alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini Lesotho kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.





Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akikutana Waziri Mkuu wa Lesotho Mhe. Samuel Ntsokoane Matekane alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.



Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akiwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Haki, Sheria na Masuala ya Bunge wa Lesotho alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akiwa na Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Makamu wa Rais Mstaafu wa Mauritius Mhe. Paramasivum Pillay Vyapoory alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.





ais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akikutana Mtukufu Mfalme Letsie wa Tatu wa Lesotho alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.




Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akiwa na Makamu wa Rais wa Seneti ya Lesotho Mhe. Tsukutlane AU alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.






Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akikutana na Mabalozi wa Uingereza na wa Umoja wa Ulaya alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakata Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akikutana wawakilishi wa Asasi za kiraia alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini Lesotho kuanzia tarehe 08 hadi 11 February.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...