Kampuni ya Bia ya
Serengeti (SBL) imeungana na wadau wa elimu wa mkoani Tanga, kupambana
na unywaji pombe kwa watu wenye umri mdogo ili kudhibiti tabia ya
unywaji pombe miongoni mwa wanafunzi wa shule.
SBL
imeshirikiana na Afisa Elimu Taaluma Sekondari wa Jiji la Tanga, Maurus
Ndunguru na Afisa Maendeleo wa Jiji la Tanga na Mratibu Mashirika ya
Kijamii Naetwa Kilango, kusambaza elimu ya kuepuka matumizi ya pombe kwa
wanafunzi katika halfa maalum iliyofanyika katika shule ya sekondari
Nguvumali.
Kampeni hiyo iliyopewa jina la SMASHED, ni kampeni ya
kupambana na unywaji wa pombe ya SBL, inayotumia michezo ya kuigiza ya
jukwaani inayowapa uezofu wa kipekee na kusisimua. Tanzania ni miongoni
mwa nchi za Afrika zenye kundi la watu wenye umri mdogo wa wanaotumia
pombe.
Utafiti uliofanywa mwaka 2019 katika mikoa ya Mwanza na
Kilimanjaro ulibaini kuwepo kwa mwenendo wa matumizi ya pombe miongoni
mwa wanafunzi wa shule za sekondari wenye umri wa miaka 15 na zaidi ni
kutoka asilimia 12.9 miongoni mwa wasichana mkoani Mwanza hadi asilimia
63.9 miongoni mwa wavulana mkoani Kilimanjaro.
SMASHED hufanyika
mashuleni na huelimisha wanafunzi wa sekondari kuhusu madhara ya
matumizi ya pombe katika umri mdogo, kwa kuwashauri kujiepusha na
matumizi ya pombe kabla ya kukomaa.
Programu hii inachanganya
matumizi ya maonyesho ya maigizo na ushiriki wa wanafunzi katika
mazingira ya motisha ya kujifunza ili kuwapa ukweli, ujuzi na ujasiri wa
kufanya uchaguzi wa kuwajibika na kuendeleza mitazamo ya uwajibikaji
katika masuala yanayohusiana na afya.
Afisa Elimu Taaluma
Sekondari wa Jiji la Tanga, Maurus Ndunguru, alipongeza SBL kwa kampeni
ya SMASHED na kutoa mapendekezo zaidi.
“Kampeni hii itasaidia sana
vijana wetu wa shule, hasa katika shule hizi tano mlizozifikia, maana
wanafunzi wamekuwa wakipata changamoto za ulevi. Nashauri pia, kampeni
hii iweze pita katika shule zote mkoani Tanga” Alisema Ndunguru.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa SBL alisema "SMASHED
inatoamafunzo muhimu juu ya athari mbaya za unywaji pombe katika umri
mdogo kwa vijana na jamii,kwa makusudi mazima ya kulinda ndoto na ustawi
wa vijana, ili kuhakikisha wanafanikiwa katika
jitihada zao".
Wanyancha
alisema mpango huo umetekelezwa nchi nzima tokea Oktoba 2022 kwa
awamu,kuanzia Dar es Salaam na kuhamia mkoani Tanga. Zaidi ya wanafunzi
15,000 wamefikiwa nampango huo katika mikoa hiyo miwili.
Afisa Maendeleo wa Jiji la Tanga na Mratibu Mashirika ya Kijamii Naetwa Kilango
amefurahishwa
na mbinu za kibunifu za utoaji elimu kwa vijana na kuwaomba wadau
wenginekubuni miradi ya kulinda ndoto za wanafunzi.
"Ahsanteni
Serengeti Breweries kwa ushirikiano wenu katika kuwaasa vijana hawa na
kuwapambinu za kulinda kesho yao. Kwa kweli vitendo vya matumizi ya
pombe katika umri mdogo ni lazima vipigwe vita na SMASHED ni jukwaa
muhimu sana", alisema Kilango.
Kwa upande mwingine, Ocheck Msuva
mwanzilishi wa asasi ya kiraia ya vijana, Bridge for Change inayotumia
sanaa ya maigizo ya jukwaani kufikisha ujumbe, amesema SBL inawapa
vijana nafasi ya kupanga kesho yao wakiwa na maarifa ya kutosha kufanya
maamuzi makini.
“Ikiwa vijana watakuwa na uelewa, maarifa na
elimu juu ya madhara ya urahibu wa vilevi ni stahiki kabisa watakuwa na
nafasi ya kufanya maamuzi sahihi ambayo ni kiini cha kuelekea katika
njia ya mafanikio.” Alisema Ocheck.
Kampeni hiyo ya SMASHED imekelezwa ndani ya shule tano za sekondari jijini Tanga, nazo ni:
Nguvumali, Kihere, Toledo, Masechu na Mnyanjari sekondari.
Waigizaji wa Maigizo ya Jukwaani, Mudrik Abdy (aliyelala), Halua Mkilindi (kulia) na Davidi Sayi (Kusho-mwisho) wakionyesha madhara ya ulevi kupitia igizo maalum, ikiwa ni sehemu ya somo katika kampeni ya kupinga unywaji pombe katika umri mdogo ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ijulikanayo kama “SMASHED”. Kampeni hiyo imefanyika katika shule tano jijini Tanga, ikiwemo Shule ya Sekondari Nguvumali, mapema leo.
Waigizaji wa Maigizo ya Jukwaani, Halua Mkilindi (kulia) na Davidi Sayi (Kusho) wakionyesha madhara ya ulevi kupitia igizo maalum, ikiwa ni sehemu ya somo katika kampeni ya kupinga unywaji pombe katika umri mdogo ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ijulikanayo kama “SMASHED”. Kampeni hiyo imefanyika katika shule tano jijini Tanga, ikiwemo Shule ya Sekondari Nguvumali, mkoani Tanga, mapema leo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nguvumali wakifurahia igizo la ucheshi la kuasa wanafunzi na matumizi ya pombe, katika kampeni ya SMASHED ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), iliyofanyika katika shule hiyo, mkoani Tanga, mapema leo.
Afisa Elimu Taaluma Sekondari wa jiji la Tanga Maurus Ndunguru (Kulia) akiongea na wanafunzi wakatika wa hafla maalum ya utoaji elimu ya unywaji pombe kwa umri mdogo ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) SMASHED. Pembeni ni Ocheck Msuva (Kushoto) Mkurugenzi wa Taasisi ya Bridge for Change inayotumia michezo ya kuigiza ya jukwaani katika kampeni ya SMASHED. Tukio hilo limefanyika katika shule ya sekondari ya Nguvumali, iliyopo Tanga, mapema leo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nguvumali, wakiangalia igizo la jukwaani la kuwaasa dhidi ya matumizi ya pombe katika umri mdogo, lililofanyika mapema leo jijini Tanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...