Na Janeth Raphael
SERIKALI imesema itaendelea kutengeneza mazingira Bora ya kujifunza katika vyuo vya ualimu kwa kuzingatia ujenzi wa majengo, utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati mbadala.

Profesa James Mdoe Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu ameyabainisha hayo leo akiwa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma katika mafunzo ya siku nne ya utunzaji mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu nchini

Profesa Mdoe amesema Serikali inatambua umuhimu na imeweka mazingira na mikakati mbalimbali ili kutunza mazingira hayo ikiwemo kutumia nishati mbadala ya kupikia ya kutumia kuni na mkaa.

"Lengo la wizara ni kuweka alama katika lengoe kuu la Taifa lautunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa kuhakikisha mafunzo yanatilewa kwa walimu mpaka kwa wanafunzi na lengi la wizara litakuwa limetimia" - Profesa Mdoe

Naye Mkurugenzi msaidizi wa Mafunzo kutoka Wizara ya elimu,sayansi na teknolojia Huruma Mageni amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa vyuo vyote 35 hapa nchini amabapo mpaka sasa vyuo 14 tayari vimeshapatiwa mafunzo hayo.

"Mafunzo haya ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu nchini ni mahususi kabisa kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuwajengea wakufunzi uelewa juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati mbadala na kupanda miti katika mazingira ya vyuo ila nao wakawafundishe walimu wanafunzi kwa ajili ya kufikisha kwa wanafunzi huko mashuleni,"amesema Mageni.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe akizungumza leo Februari 23,2023, Mpwapwa , Mkoani Dodoma, wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu hapa nchini (TESP).
Mkurugenzi msaidizi wa Elimu ya Ualimu kutoka Wizara ya elimu,sayansi na teknolojia Huruma Mageni,akizungumza leo Februari 23,2023, Mpwapwa , Mkoani Dodoma, wakati  akitoa taarifa ya  mafunzo ya siku nne ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu hapa nchini (TESP).
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya siku nne ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu hapa nchini (TESP), yanayofanyika Mpwapwa, Mkoani Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Prof.James Mdoe katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku nne ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu hapa nchini (TESP), yanayofanyika Mpwapwa, Mkoani Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...