Mratibu Mtandao unaojihusisha na masuala ya maendeleo na ukuaji wa kiuchumi na unaohusisha wataalamu waliobobea kwenye maswala ya kuibua na kufuatilia ukuaji maswala ya kiuchumi Barani Afrika (Accelerate Africa), Kanda ya Afrika Gilbert Ewehme akizungumza na wafanyabiashara wadogo na wa kati wakati wa uzinduzi wa mtandao huo uliofanyika leo Februari 23, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Accelerate Africa nchini Tanzania Pendo Lema,
akizungumza na wafanyabiashara wadogo na wa kati wakati wa uzinduzi wa mtandao huo uliofanyika leo Februari 23, 2023 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo na wa kati wakifuatilia hotuba ya Gilbert Ewehme, ambaye ni mratibu wa Accelerate Africa kanda ya Afrika wakati wa zinduzi wa Mtandao unaojihusisha na masuala ya maendeleo na ukuaji wa kiuchumi na unaohusisha wataalamu waliobobea kwenye maswala ya kuibua na kufuatilia ukuaji maswala ya kiuchumi Barani Afrika (Accelerate Africa)

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MTANDAO unaojihusisha na maswala ya maendeleo na ukuaji wa kiuchumi na unahusisha wataalamu waliobobea kwenye maswala ya kuibua, kufuatilia ukuaji maswala ya kiuchumi Barani Afrika (Accelerate Africa) umezindua rasmi shughuli zake nchini Tanzania.

Hatua hiyo, iliyofanyika leo Februari 23, 2023 jijini Dar es Salaam unaifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu kufanya uzinduzi huo kati ya mataifa 10 ambayo yanaunda mtandao huo ikitanguliwa na Cameroon pamoja na Rwanda.

Katika mkutano huo, wafanyabiashara wadogo na wa kati kutoka sekta mbalimbali wamekutana kujadili, kubadilishana na kushauriana kuhusu maswala yanayohusiana shughuli za kifedha, uwekezaji na uanzishaji wa viwanda kuelekea ushiriki wao katika Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA).

Akizindua mtandao huo, Mratibu wa Accelerate Africa kanda ya Afrika Gilbert Ewehmeh amesema, “Mfumo wetu huu unalenga kuunda biashara endelevu kwa nia ya kuimarisha sekta ya viwanda ili kuondoa umasikini na kuhakikisha uwepo wa uchumi endelevu.”

Amesema mtandao huo umejikita zaidi Barani Afrika kutokana na ukweli kuwa changamoto zinazohusiana na maswala ya kiuchumi barani humo hazitofautiani na kwamba ni wakati muafaka kwa wanachama kutumia fursa zinazotokana na eneo huru la Biashara la Bara la Afrika ambazo amesema nchi nyingi hazina ufahamu kuhusiana na fursa hizo.

"Lazima tuanze na vikundi vya wafanyabiashara wadogo na wale wa kati kwani wengi wao bado hawana uelewa wa fursa nyingi za biashara zilizoko na ambazo wakizifahamu na kuzitumia watanufaika zaidi.” Amesema

Uzinduzi huo umeenda sambamba na mkutano wa kwanza wa wafanyabiashara wadogo wanaonza kuwekeza na wale wa vikundi vya Wafanyabiashara wadogo na wa kati.

Kwa upande wake Mratibu wa Accelerate Africa nchini Tanzania Pendo Lema, amesema hatua hiyo mpya itawasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kuchangamkia fursa zilizoko kwa kupata uelewa wa kutosha kuhusiana na maendeleo ya kibiashara ulimwenguni.

"Accelerate Africa inatarajia kufanya mkutano mkubwa Mwezi Juni 2023, ambapo nchi zote wanachama watalazimika kuchagua wawakilishi watatu kila mmoja; hapa nchini wawakilishi hao itabidi wapatikane kwa njia ya ushindani utakaoandaliwa na mamlaka husika."amesema.

Aidha mtandao huo pia una mpango wa kuanzisha programu itakayojulikana kwa jina la ‘Operesheni ya mafunzo kwa wajasiriamali 100’ ambayo pamoja na mambo mengine italenga kuwapa washiriki kupata ufadhili wa kifedha, lengo kuu ni kuhakikisha kila nchi mwanachama inakuwa na wafadhili wa uhakika.

Nchi zingine zilizopo kwenye umoja huo ni pamoja Botswana, Malawi, Ghana, Afrika Kusini, Uganda, Kenya na Zimbabwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...