Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya Sportpesa imedai kusikitishwa na uamuzi wa uongozi wa Klabu ya Yanga kukiuka makubaliano ya mkataba wao baada ya kuzindua Jezi mpya zenye Mfadhili mwingine.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo, imedai kuwa ombi la Yanga SC kutafuta Mfadhili mwingine kwa ajili ya mashindano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) hatua inayofuata, lilikuwa ni kukiuka makubaliano ya kimkataba baina yao, huku wakieleza kuwa, wana haki ya pekee ya kuwa kifuani kwa kuwa wao ni Wadhamini wakuu wa Klabu hiyo.

“Sportpesa inafahamu kikamilifu maagizo na masharti ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuhusu utangazaji au ufadhili uliopo na ilikuwa imetumia kaulimbiu ya ‘Visit Tanzania’ kuchukua nafasi yetu ili kufuata masharti yanayohitajika kutoka CAF,” imeeleza taarifa hiyo.

Sportpesa imeeleza kuwa kampeni hiyo ya ‘Visit Tanzania’ ilifanikiwa kuitangaza nchi, Kimataifa katika misimu miwili kupitia Michuano hiyo ya CAF, Sportpesa imedai kuwa pendekezo lao kwa Yanga SC lilikataliwa kwa kuwa Klabu hiyo iliamua kuuza haki hizo bila kujali masharti ya kimkataka yaliyopo baina yao.

Hata hivyo, Sportpesa imedai kuhifadhi haki yake na kuomba fidia na msaada kutoka Mamlaka husika kutokana na uharibifu uliosababishwa, Sportpesa inaamini kuwa bado ni Mdhamini Mkuu wa Klabu ya Yanga na ina haki ya kipekee ya kuwa kifuani mwa Jezi za timu hiyo kuanzia 2022 hadi 2025.

Januari 30 mwaka huu, Yanga SC ilizindua Jezi zao mpya kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC), hatua ya makundi huku Jezi hizo zikiwa na Mdhamini mwingine tofauti na Mdhamini wa sasa ambaye ni Kampuni ya Sportpesa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...