
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
SHIRIKISHO la Soka duniani (FIFA) limethibitisha kuwa kwa mara ya kwanza, Waamuzi watakaoamua michezo ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya vilabu watawasiliana moja kwa moja na watazamaji watakuwepo uwanja na nyumbani, wakati Waamuzi hao wakiwa uwanja kuamua michezo husika, pindi wakiwa wanatumia msaada ya VAR.
Kupitia mitandao yao ya kijamii, Shirikisho hilo na Rais wake, Gianni Infantino wamethibitisha hilo. FIFA na Rais wake wamesema watazamaji waliopo uwanjani na wale wanaotazama kupitia Runinga, nyumbani watapata fursa ya kuzungumza moja kwa moja na Mwamuzi ambaye yupo uwanjani anaamua pambano wakati huo huo yeye akitumia kipaza sauti chake (Microphone) akiwa kwenye VAR.
“Kwa mara ya kwanza, Mwamuzi atazungumza moja kwa moja na mashabiki uwanjani na watazamaji wa Runinga nyumbani kupitia kipaza sauti cha Mwamuzi huyo, akielezea kwa nini uamuzi umefanywa. Hii ni sehemu ya majaribio ya FIFA kwani tunataka kila wakati kuboresha uwazi na ubayana wa VAR na kuboresha elimu. Tunaamini mtaipenda!,” amesema Rais wa FIFA, Gianni Infantino.
Infantino amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuwepo uwazi zaidi juu ya maamuzi ya waamuzi hao. Hata hivyo amesema jaribio hilo litaanza kwenye Michuano ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya Vilabu (FIFA Club World Cup) nchini Morocco kuanzia Februari 1 hadi Februari 11, 2023.
Michuano hiyo ya dunia kwa ngazi ya Klabu itafanyika nchini Morocco huku timu saba katika Mabara saba duniani zitashiriki, timu hizo ni Wydad Casablanca, Al Ahly SC, Real Madrid, Auckland City FC, Seattle Sounders FC, Al Hilal SFC na CR Flamengo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...