Serikali itaendelea kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini kwa manufaa ya maendeleo ya taifa kwa ujumla.


Hayo yameelezwa na Waziri wa Usafirishaji na uchukuzi, Profesa Makame Mbalawa wakati wa uzinduzi wa Nembo ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) leo Februari 3, 2023. Amesema kuwa uzinduzi wa nembo hiyo uakisi utendaji na utekelezaji wa malengo Mamlaka hiyo kwa kuongeza tija katika usafiri wa anga hapa nchini.

Amesema kuwa serikali imekuwa ikitenga fedha na kuhakijiasha kunakuwa na huduma bora, kuboresha miundombinu ya Viwanja vya ndege na kuimarisha usalama na kuwa bora kulingana na viwango vya kimataifa.

Prof. Mbalawa amesema kuwa maboresho ya Mifumo ya Malipo na jitihada zilifanywa na TAA yatavutia uwekezaji na kuongeza uwiano wa mapato yasiyotokana na shughuli za anga kwa lengo la kuvutia wawekezaji katika viwanja vya ndege nchini kote.

Aidha Prof. Mbalawa amekata utepe kuashira uzinduzi wa magariyakiwemwo magari mawili ya kusafirisha wagonjwa wanaopita au walinaopata changamaoto za kiafya katika viwanja vya ndege pamoja na jengo la watu mashuhuri (VIP)

Pia ametoa rai kwa watumiaji wa magari hayo watumie kwa umakini ili yadumu muda mrefu.

"Hivi sasa tunampango wa kuweka taa za kuongozea ndege katika Uwanja wa ndege wa Msalato Dodoma ili kuhakikisha viwanja vyote vya ndege vinafanya kazi masaa 24, kama viwanja vyote vya ndege vingekuwa vinafanya kazi saa 24 biashara ya ndege ingebadilika... Na uchumi wetu ungebadilika." Amesema Prof. Mbalawa

Amesema kuwa Wizara ya usafirishaji na Uchukuzi itahakikisha viwanja vyote vya ndege vinakuwa na taa ili ndege ziwe zinaruka na kutuma masaa 24.

Licha ya hayo Prof. Mbalawa amewapongeza Uongozi wa TAA pamoja na wafanyakazi zote kwa kazi wanaoyoifanya pamoja na kuwa wabunifu katika kuendeleza na kuboresha Miundombinu ya usafiri wa anga Nchini.

Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara Usafirishaji na Uchukuzi Dkt. Ally Possi amesema kuwa nembo iliyozinduliwa leo iwe dira mpya katika Utendaji wa TAA, nautendaji Mpya wa mamlaka hiyo.

Pia amewaasa kutumia vizuri ubora wa nembo katika Kutoa huduma bora zaidi.

Picha za matukio


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...