TAMASHA la ''Lady in Red'' lafanyika Dar wabunifu na wanamitindo chipukizi wapatiwa tuzo kama pongezi ya Sekta ya ubunifu na wanamitindo kutambua mchango wao.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Hugo Domingo, Mario Frenandes akizungumza wakati wa tamasha hilo amesema kuwa waandaji wa onyesho hilo kwa Msimu wa pili  wa "Lady in Red limekuwa moja ya jukwaa linalotoa fursa mbalimbali sekta ya ubunifu,wanamitindo, mapambano na Muziki.

"Huu ni msimu wa pili tunaendelea kuunga mkono jukwaa hili lengo ni kuwapa nafasi wenye vipaji kuonekana katika sekta mbalimbali na ndio hasa lengo la Hugo Domingo kuona vijana wanafanya kazi kutokana na ujuzi wao na hata kwenye Tamasha hili hatukubagua tumeshirikiana nao wanamuziki,washereheshaji na wasanii.

Fernandes amesema Tamasha hilo kwa mwakani wanatarajia kufalifanya kwa ukubwa sana na kushirikisha wabunifu kutoka nje huku Tamasha likitarajiwa kufanyika Visiwani zanzibar.

Ameeleza namna jukwaa hilo kwa mwaka huu kutimiza kwake miaka 20 tangu kuasisiwa na Mbunifu Mkongwe Mama Asia Khamsin imepelekea wao kama waandaaji wa jukwaa hilo kwa utofauti na kwa ukubwa zaidi .

"Mitindo sasa hivi inafanya vizuri mwakani tuna mpango wa kuanza visiwani Zanzibar na kilele chake kumalizika Dar es Salaam, hivyo wabunifu wajiandae kuonyesha mavazi yenye viwango vya juu zaidi."
Pia ameongeza kuwa wadau mbalimbali wa sekta ya Mitindo wa endelee kuunga mkono Tamasha hilo ili liendelee kuwepo kila mwaka kwa lengo la kuwaunga mkono wabunifu chipukizi pamoja na wanamitindo.

Katika Tamasha hilo liliweza kutoa tuzo ya Heshima kwa Muasisi wa tamasha hilo Mama Asia Idarous Khamsin kwa kuanzisha tamasha hilo miaka 20 iliyopita na kutoa vipaji vingi ambavyo kama vile  Ally Rhemtula, Miriam Odemba, Khadija Mwanamboka, Mustafa Hassanali, Martin Kadinda, Flaviana Matata, Ria Fernandes, Victoria Martin na wengine wengi
 
 
Miaka ya hivi karibuni Asya Idarous Khamsin alianzisha ushirikiano na kampuni ya Hugo Domingo Limited, kampuni maarufu ya upambaji yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam ikiwa na Ofisi pia Arusha, Dodoma, Mwanza, Zanzibar na ikiwa na Mahusiano pia na nchi mbalimbali za Afrika.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...