Mhadhiri wa Sera Ufatiliaji na Tathmni wa Chuo Kikuu Dkt.Francis Mwaijande akizungumza na wadau wa Utalii kutoka sekta mhimu katika masuala ya utalii wakati wa kutoa mafunzo yaliyotolewa na Tanzania Evaluation Association (TanEA) mafunzo yaliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kwa siku tano.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Maliasili na Utalii, Cyrus Kapinga akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya kutathmini na Kufuatilia mradi wa REGROW yanayotolewa na Tanzania Evaluation Association (TanEA) mafunzo yaliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam, ya Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Coretha Komba akizungumza wakati wa kuwakaribisha wadau wa masuala ya utalii wakati wa kupewa mafunzo ya Kutathmini Mradi wa REGROW, mafunzo yanayofanyika Ndaki ya Dar es Salaam.
Baadhi ya Wadau wa utalii wakichangia mada wakati wa mafunzo ya kutathmini Mradi wa REGROW.
Wa kwanza Kulia, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Maliasili na Utalii, Cyrus Kapinga akisikiliza mada wakati wa mafunzo.
Wadau wa Masuala ya Utalii wakisikiliza mada.
Picha ya Pamoja.
KATIKA kuhakikisha Serikali inafanikisha Malengo yake ya kukuza sekta ya Utalii nchini, Tanzania Evaluation Association (TanEA) na Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, wametoa mafunzo ya siku tano kwa wadau wa masuala ya Maliasili na Utalii ili kuboresha usimamizi Ufatiliaji na Kutathmni Mali zake hapa nchini.
Akizungumza na Mwandishi wetu mara baada ya mafunzo hayo, Mhadhiri wa Sera Ufatiliaji na Tathmni wa Chuo Kikuu Dkt.Francis Mwaijande amesema kuwa wadau kutoka sekta mbalimbali za Wizara hiyo ili waweze kufanikisha malengo ya Wizara na Taifa kwa Ujumla.
Amesema kuwa Mafunzo hayo yanayotolewa kwa ajili ya kwenda kusimamia na kutathmini mradi wa Resilient Natural Resources Management for the Tourism Growth (REGROW) kwa ajili ya kukuza Utalii hapa nchini.
Wadau hao ni kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Hifadhi za Taifa (TANAPA), Taasisi ya utafiti wa wanyama Pori (TAWIRI), Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Bodi ya Bonde la Maji Mto Rufiji(RBWB).
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Maliasili na Utalii, Cyrus Kapinga amesema kuwa wadau hao wanajifunza namna ya kutathmini na kusimamia Mradi wa REGROWambao utaenda kukuza utalii katika maeneo ya kusini mwa Tanzania.
Amesema kuwa mafunzo hayo yakawasaidie katika kutekeleza Mradi wa REGROW na miradi mingine ambayo itakuwa inatekelezwa na Serikali.
Kwa upande wake mnufaika wa mafunzo hayo, Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mradi wa REGROW, Michael Karaghe amesema kuwa “Mwanzo hatukuwa na mafunzo ambayo tumepewa hapa leo, tulikuwa tunakagua tuu kama mazoea, lakini kwa kupitia mafunzo haya yanatusaidia kama sisi maafisa mradi tunao husika moja kwa moja na ufatiliaji na tathmini kutujengea uwezo wa kukagua kulingana na miongozo ya serikali, lakini pia itatusaidia kuangalia thamani ya fedha ambayo serikali imetoa kwa ajili ya kutekeleza mradi huu wa REGROW na inafanya kazi kulingana matarajio yaliyowekwa.
Naye, Loramatu Meikoki Afisa Mafunzo wa Mradi wa REGROW, amesema kuwa Mradi wa REGROW ulianza tangu Mwaka 2017 na ulitakiwa kumalizika mwaka 2023 ila kutokana na changamoto za UVIKO 19 wameongezewa muda na wanatakiwa kuukamilisha mwaka 2025.
Amesema maeneo yanayofikiwa na mradi huo ni katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Udzungwa, Mikumi, na hifadhi ya Nyerere ambapo hifadhi hizo zote zipo kusini mwa Tanzania.
Meikoki ameeleza kuwa katika hifadhi hizo za taifa mambo mbalimbali yatafanywa ikiwemwo kutengeneza miundombinu ya barabara madaraja, ujenzi wa Nyumba za Kulala watalii, ukarabati wa Viwanja vya Ndege na kununua Magari kwaajili ya shughuli za Utalii pamoja na kusaidia jamii zinazozunguka katika hifadhi hizo.
Amesema mafunzo hayo yatawajengea uelewa wa jinsi ya kusimamia Ufuatiliaji na tathmini ya mradi wa mzima katika maeneo hayo ikiwa pamoja na kutathmini fedha zilizotumika na miundombinu iliyopo kulingana na matakwa ya Serikali.
Amesema kuwa mafunzo hayo yataisaidia serikali kuhakikisha matarajio waliyojiwekea yanafanikiwa kwa wakati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...