KAMPUNI Ya mafuta ya TotalEnergies Tanzania imesherehekea siku ya wapendao Valentine's Day na watanzania wakiwemo wateja kwa kuhamasisha upendo na kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo washindi wa droo ya 'Valentine Promotion ' ambao wamepata fursa ya kufurahia siku hiyo kwa kupata chakula cha usiku katika moja ya hoteli ya hadhi ya nyota tano Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la ugawaji zawadi kwa wateja waliokuja kupata huduma katika kituo cha TotalEnergies Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Meneja wa maduka ya TotalEnergies 'Bonjour' Jane Mwita amesema, kupitia droo ya 'Valentine Promotion' iliyoanza Februari 2 hadi 13 iliendeshwa katika vituo vya mafuta vya TotalEnergies na wateja walionunua bidhaa za thamani ya kuanzia shilingi elfu hamsini na kuendelea waliingia katika droo hiyo washindi kupatika.
"TotalEnergies inawapenda na kuwathamini wateja, tunafurahi nao katika siku hii ya wapendao kwa kutoa zawadi mbalimbali na kubwa zaidi ni kuwasihi kuendelea kutumia mafuta bora yenye kiambata cha Excellium na bidhaa bora na salama za vilainishi." Amesema.
Amesema, kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma zenye viwango bora pamoja na kurudisha kwa wateja na jamii inayonufaika na huduma bora inayotolewa na TotalEnergies Tanzania.
Kwa upande wake Meneja Mosoko wa TotalEnergies Caroline Kakwezi amesema, katika msimu huu wa sikukuu ya wapendao kampuni hiyo inasambaza upendo kwa wateja wao kwa kutoa zawadi mbalimbali.
"Vituo vya TotalEnergies ni one stop center wateja wetu wakitembelea vituo vyetu leo watapata zawadi na wataweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo kujaza mafuta, kufanya service ya magari, kuosha magari pamoja na kununua bidhaa katika maduka ya Bonjour." Amesema.
Pia amesema kampuni hiyo imeendea kuwa kinara kutokana na upekee wa utoaji huduma kwa kuzingatia ubora na usalama kwa watumiaji hususani huduma ya mafuta (Total Excellium) yenye viambata vyenye kusafisha injini za vifaa vya moto na kutumia mafuta kidogo na kwenda umbali mrefu.
Baadhi ya wateja walioshinda na kupata fursa ya kupata chakula cha jioni katika moja ya hoteli yenye hadhi ya nyota tano ni pamoja na Abdul Hamis kutoka Bagamoyo, Pwani na Godfrey Mushi wa Dar es Salaam huku wateja waliotembelea na kujaza mafuta katika kituo hicho wakijipatia zawadi ya Chokoleti ya Cadbury.
Meneja Mosoko wa TotalEnergies Tanzania Caroline Kakwezi (katikati,) akiendesha zoezi la kuwatafuta washindi wa 'Valentine Promotion'' washindi hao wamepata fursa ya kupata chakula cha jioni katika moja ya hoteli yenye hadhi ya nyota tano, kushoto ni Ofisa Mawasiliano wa TotalEnergies Anita Bulindi, Leo Jijini Dar es Salaam.Meneja wa Maduka ya TotalEnergies Jane Mwita akizungumza na baadhi ya wateja waliotembelea kituo cha mafuta TotalEnergies Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Maduka ya TotalEnergies Jane Mwita akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hafla hiyo na kueleza kuwa TotalEnergies itaendelea kutoa huduma zenye viwango bora zaidi kwa wateja na watumiaji wa bidhaa, Leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...