Na Janeth Raphael
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, amewaonya watendaji wa kata kuacha kuwa miungu watu kwa kuwakamata wananchi na kukamata mali zao kwa uonevu bila kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za kazi.

Ameyasema hayo leo tarehe 14 Februari, 2023 Jijini Dodoma kwenye hafla ya kukabidhi magari kwa Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(T
ARURA) na pikipiki kwa watendaji wa kata.

Amesema kuwa kumekuwemo na malalamiko kuhusu ukiukwaji wa maadili ya uongozi wa umma unaofanywa na Watendaji wa Kata hivyo amewataka kuhakikisha wanasimamia Sheria bila kuonea wananchi

“Msijifanye miungu watu kwa kuwakamata wananchi na kupora mali zao kwa uonevu, simamieni sheria lakini msionee watu, sisi huku juu tunaletewa tuhuma nyingi za ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma ambazo zinafanywa na baadhi yenu Maofisa Watendaji wa Kata,”amesema

Dkt. Mpango amewataka Watendaji wa Kata wote nchini kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi, uaminifu kwa kuwa ndio kiungo muhimu kati ya Serikali na wananchi.

Amewataka Wakurugenzi wote nchini kufuatilia tuhuma hizo na kuchukua hatua stahiki za kisheria na kinidhamu.

Ameeleza kuwa kazi ya Mtendaji wa Kata ni kumsaidia Mkurugenzi wa Halmashauri katika kusimamia shughuli za maendeleo katika kata zao, hivyo amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanawasimamia Watendaji wa Kata katika kutekeleza majukumu yao yakiwemo ufanyikaji wa vikao na mikutano ya Kisheria.

Kuhusu ugawaji wa Pikipiki Dkt. Mpango amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanagawa pikipiki hizo kwenye kata zilizopo pembezoni na kata zenye maeneo makubwa ili kuweza kuwafikia wananchi kwa urahisi.

Naye, Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikubali pendekezo la kutumika Sh.Bilioni 2.9 za mgao wa kodi ya majengo kuanzia Julai, 2021 hadi Februari, 2022 ili kununua vitendea kazi hivyo kwa watendaji wa kata.

Aidha, amesema pikipiki hizo zitaongeza idadi ya watendaji wenye vitendea kazi hivyo kuwa zaidi ya 1,500 kati ya kata 3,956 zilizopo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akihutubia Viongozi na Watumishi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 54 kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Hafla iliofanyika katika ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma – Mtumba leo tarehe 14 Februari 2023.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angella Kairuki akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi magari kwa wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) na pikipiki kwa watendaji wa kata.
Sehemu ya viongozi mbalimbali waliohudhiria hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo wakati akijaribu moja kati ya magari 54 yaliokabidhiwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) katika hafla iliofanyika katika ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma – Mtumba leo tarehe 14 Februari 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Afisa Mtendaji Kata ya Ng’ong’ona (Kulia) iliopo Dodoma moja kati ya Pikipiki 916 zilizotolewa kwa Watendaji Kata kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, katika hafla iliofanyika katika ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma – Mtumba leo tarehe 14 Februari 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...