Na Mwandishi Wetu Michuzi TV- Morogoro

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amesema atakwenda kumwambia Rais Samia Suluhu Hassan hakuna chochote kimefanyika katika kituo cha afya Kinole mkoani Morogoro na watahakikisha hadi Aprili mwaka huu ujenzi wa kituo hicho unaanza huku akisema wanataka huduma za afya kwa wananchi  isiwe anasa.

Akizungumza leo Februari 3,2023 na wananchi wa Kinole mkoani Morogoro akiwa kwenye  kukagua utekelezaji wa Ilani pamoja na uhai wa Chama hicho, Chongolo amesema atakwenda kumueleza Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kituo cha afya Kinole kwa kuwa watu wanahitaji kituo hicho.

“Kwasababu kutoka hapa kwenda mjini ukiwa na ujauzito ni mateso makubwa , lakini niseme nilijuaje Kinole kuna shida ya afya , kuna siku nilimuita Waziri wa Afya ofisini kwangu lakini baada ya kuingia nikaona wameingia na wabunge wengine wawili akiwemo Mbunge wenu.Nikamuuliza amefuata nini akasema anataka kumuona Waziri.

“Nilipomuuliza anataka kusema nini ndipo mbunge wenu akanieleza kuhusu kuongezewa fedha za Hospitali ya Wilaya ili kukamlisha majengo yote likiwemo la Monchwari pamoja na miundombinu mingine.Pili akaomba fedha za kituo cha afya Kinole zirudishwe kwasababu zilishakuja zikaondoshwa na hivyo kituo hakikujengwa, hivyo  tukakubaliana na Waziri aende akahangaike na bajeti ili kituo cha Kinole kipate fedha kwa ajili ya kujenga kituo hicho,”amesema Chongolo.

Amesema amepata taarifa tayari eneo kwa ajili ya kujenga kituo hicho lipo baada ya wananchi kuamua kujitolea hivyo akawahakikishia ndani ya miezi miwili kuanzia sasa fedha zitakuwa zimefika kwa ajili ya kuanza ujenzi.

“Tunataka huduma ya afya kwa wananchi isiwe anasa, tunataka akina mama wajifungue bila mateso , akitoka kujifungua akirudi nyumbani amwambie baba ana hamu ya kurudi kule, “amesema Chongolo.

Kuhusu elimu, Chongolo amesema bado kuna changamoto ya kupeleka mtoto wa kike kusoma , na jamii inaona kama vile mtoto anayestahili kusoma ni wa kiume peke yake jambo ambalo sio sawa na wenye dhana hiyo hawafanyi vizuri.“Pelekeni watoto wa kike wakasome, tunataka wakuu wa mikoa watoke Kinole.”


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema akiwasalimia wakazi wa Kinole akiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo.Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ameongozana pia na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu) pamoja na Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali ambapo ziara hii ina lengo la Kukagua, Kuhimiza na Kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na  wakazi wa  Kinole, Morogoro Vijijini mkoa wa Morogoro.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu) pamoja na Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali ambapo ziara hii ina lengo la Kukagua, Kuhimiza na Kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025

 Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu)  akiwasalimia wananchi wa Kinole.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema akisonga ugali kwenye moja ya banda la Mama Lishe katika kijiji cha Kinole,Morogoro Vijijini leo Februari 3,2023 walipofika na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu) pamoja na Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali  kwenye ziara yao ya siku tisa yenye lengo  Kukagua, Kuhimiza na Kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025

Pichani juu (wa pili kulia) Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akiwa na Mbunge wa Jimbo la Morogro Kusini Mashariki Mhe.Hamis  Taletale pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu)  wakipata chakula kwa pamoja katika moja ya banda la Mama Lishe mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa Kinole,Morogoro Vijijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...