Na Mwandishiwa Wetu

MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewaomba watumishi wa umma wilayani hapo kudumisha umoja na ushirikiano ili kuchochea maendeleo.

Mgeni amesema hayo wakati akizungumza na wakuu wa idara pamoja na taasisi mbalimbali Wilaya ya Same mara baada ya kupokelewa.

Aidha ametoa shukrani za dhati kwa wakuu wa idara kwa mapokezi makubwa ambayo amekutana nayo na kuahidi kushirikiana nao ili kuipaisha Same katika sekta za kijamii, kiuchumi na maendeleo.

Amesema mapokezi hayo hakuyatarajia na kusema hii inaonesha mshikamo mkubwa uliopo kwa viongozi hao katika uwajibikaji wa kazi huku akiwaomba wakuu wa idara zote kuendelea kushirikiana kwa pamoja lengo ni mkusaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia wananchi na kusimamia miradi yote ambayo inayoendelea kwenye wilaya hiyo.

Kwa upande wake aliyekuwa DC wa Same, Edward Mpogolo amewaomba wakuu wa idara zote kumpa ushirikiano wa kutosha mkuu wa wilaya mpya na kuonyesha uzalendo kwa Taifa na wananchi kwa ujumla.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...