Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Manachama wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 06, 2023 jijini Dar es Salaam. mara baada ya kuzindua JukwaaMajadiliano Wilaya ya Ilala.
Mkurugenzi wa TCD, Bernadetha Kafuko, Akitoa ufafanuzi juu ya Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) jijini Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Majadiliano Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari06, 2023.
 Msaidizi wa Masuala ya Siasa na Uchumi, Ubalozi wa Marekani, Bion Bliss akizungumza wakati wa wa Uzinduzi wa Jukwaa la Majadiliano Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari06, 2023.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Majadiliano Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari06, 2023.





Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa wa Wilaya ya Ilala wakiwa katika Uzinduzi wa Jukwaa la Majadiliano Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari06, 2023.
 
Picha za Pamoja.

VIONGOZI wa Vyama vya siasa nchini wameaswa kushirikiana ili waweze kujenga mazingira mazuri ya kufanya siasa zenye tija na za kushindana kwa hoja.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Profesa Ibrahim Lipumba leo Februari 06, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua Jukwaa la Majadiliano Wilaya ya Ilala kwa lengo la kuwaunganisha viongozi wa vyama vya Siasa katika wilaya hiyo kwaajili ya kuanza majadilia ya pamoja katika kuunda mshikamano na umoja.

Amesema Jukwaa hilo litawezesha majadiliano na jinsi ya kuendeleza Demokrasia, Amani na kuendeleza maendeleo ya taifa kwa Ujumla.

“Kitaifa tunajukwaa la vyama, tunakutana na viongozi wa Vyama vya Siasa kwa ngazi ya Wilaya ili kuendeleza Demokrasia na kuweza kubadilishana mawazo ni namna gani ya kuendeleza Demokrasia na kuweza kujadiliana namna ambavyo shughuli zetu za kisiasa tunazifanya kwa mujibu wa taratibu na sharia na kwaamani.” Ameeleza Prof. Lipumba

Katika jukwaa hilo wamesisistiza kwamba mambo ya msingi hasa kuwepo ni kuwa na tume huru ya uchaguzi, nimhimu ili tuweze kuwa na amani endelevu.

“Kama nchi na taifa tunahitaji kujadiliana ili tuweze kuapata tume huru ya uchaguzi ambayo itakuwa na uwezo wa kusimamia chaguzi za serikali za mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025.” Ameeleza Prof. Lipumba

Amesema hayo ndio mambo ya kitaifa na jukumu la Serikali katika hatua ya Wilaya, tunahitaji viongozi wetu wa vyama waweze kushirikiana kujenga mazingira mazuri ya kufanya siasa zenye tija, siasa za kushindana kwa hoja.

Pia Prof. Lipumba amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuwa na maridhiano ya majadiliano na vyama vya siasa nchini ikiwa ni pamoja na kuruhusu vyama vya Siasa Nchini vifanye kazi zake kwa uhuru na Amani.

Amesema Rais Dkt. Samia ameruhusu Mambo mamne katika utekelezaji wa kazi za vyama vya siasa katika vipengele vine ambavyo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko na Ujenzi mpya wa Taifa.

Kwa Upande wa Msaidizi wa Masuala ya Siasa na Uchumi, Ubalozi wa Marekani, Bion Bliss amesema kuwa Marekani inashirikiana na washirika wake katika kuhakikisha demokrasi inaimarika, wanachi wanakauli na kuweza kuchagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi huru, Amani, haki na uaminifu.

Amesema jukuwaa hili litawanguanisha Viongozi wa vyama vya siasa ili kuweza kuafanya siasa,Kuwa na vipaumbele vya pamoja ikiwemwo mazungumzo ya pamoja ili kuleta uelewa wa pamoja kwa wananchini wake.

Akizungumzia kuhusiana na majadiliano ya pamoja na viongozi wa vyama vya siasa, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa Jukwa hilo litakuwa eneo mhimu la kuwaweka pamoja viongozi wa vyama vya siasa ili kujadiliana changamoto mbalimbali na kuweza kupata majawabu wakiwa Mezani.

“Naamini kwamba Chini ya Uongozi wa TCD chini ya Mwenyekiti wake, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti, Prof. Lipumba nchi hii itakaa kwenye meza ya majadiliano ya pamoja, tuwaombee kuelekea kwenye maridhiano na majadiliano.” Amesema Zitto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...