Na Karama Kenyunko Michuzi TV
WAFANYABIASHARA wa tatu wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Kisitu wakikabiliwa na shtaka moja la kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya Heroin
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Tumaini Maingu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Amiri Msumi imewataja washtakiwa hao kuwa ni Ramadhani Gumbo, Fahadi Swalehe na Ashrafu Hamisi
Inadaiwa kuwa, Julai 3, 2019 huko Mbezi eneo la Kwembe lililoko ndani ya Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa walikutwa wakifanya biashara ya dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa kilogramu 21.67.
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na muda wowote taarifa zitafika Mahakamani kwani walikuwa wakisubiri mabadiliko ya hati ya mashitaka.
Wakili anayewatetea washtakiwa, Abdillah Abdulaziz ameiomba Mahakama kutenda haki kwa washtakiwa kwani wemekaa ndani kwa muda mrefu na mara zote wamekuwa wakiambiwa kuwa upelelezi umekamilika.
“Mheshimiwa hili shauri ni jipya lakini sio jipya na muda sio mrefu limetoka kufutwa kwa mheshimiwa Shahidi, linaenda mwaka wa nne sasa na mara zote upande wa mashtaka umekuwa ukisema upelelezi umekamilika, naomba haki itendeke ili washtakiwa hawa wajue hatma zao” amesema Abdillah.
Kesi hiyo imehairishwa hadi Machi 14 mwaka huu itakaporudi tena kwa ajali ya kutajwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...