Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

Ofisa Elimu Mkoa wa Pwani ,Sara Mlaki ametoa rai kwa walimu wa awali ,kufanya mabadiliko katika ufundishaji na ujifunzaji kwenye shule za awali pamoja na unaboreshwa ili kutokomeza changamoto ya kutokujua kusoma,kuandika,na kuhesabu (KKK) katika Mkoa wa Pwani.

Aidha amepongeza walimu hao kwa kazi kubwa ya Zoezi la uandikishaji wanafunzi kujiunga na madarasa ya awali ambapo hadi sasa mkoa umefikisha asilimia 120 sanjali na upatikanaji wa Chakula kwa wanafunzi shuleni.

Akifungua semina ya siku tano kwa walimu , kupitia Mradi wa shule Bora inayojumuisha jumla ya halmashauri 9 ndani ya mkoa wa Pwani ikiwa na jumla ya Washiriki 120 katika Shule ya Sekondari Bagamoyo Mkoani Pwani.

‘’Naamini kupitia semina hizi mtapata nafasi nzuri ya kukaa pamoja na kuanza kutatua changamoto zilizopo ili kuweza kusaidia watoto wa madarasa ya awali na kuanza kuona sasa Madarasa hayo yanazungumza kwa vitendo’’alifafanua Sara .

Aliwaomba walimu hao, kuendelea kusaidia kutatua changamoto za ufundishaji na ujifunzaji kwa Madarasa ya awali katika maeneo yao.

Pamoja na hayo ,Sara alieleza mkoa huo umejipanga kupimana katika ngazi zote ili kuleta matokeo chanya ya semina ambazo tayari zimeanza kutolewa pamoja na kuongeza ufaulu na kuhakikisha wanafunzi wote wanajua kusoma kuandika na kuhesabu, kwani moja ya sababu zilizochangia kushuka kwa kiwango Cha ufaulu matokeo ya elimu ya msingi kimkoa 2022,ni watoto kutokujua kusoma kuandika na kuhesabu.

Mafunzo hayo ya siku tano ,yamejumuisha shule zipatazo 40 ,walimu waliohudhuria 120 Mkoani Pwani.

Mradi wa shule bora ni program ya Serikali ya Tanzania ya kuboresha elimu ya awali na msingi kwa ufadhili wa Ukaid na Serikali ya Uingereza inayotekelezwa katika mikoa Tisa Tanzania Bara.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...